Wakati timu ya mpira wa miguu ya
Tanzania ‘Taifa Stars’,kikitarajiwa kuingia kambini leo Machi 19, 2017
kwenye Hoteliya Urban Rose, Dar es Salaam, kikosi hicho cha Kocha Salum
Mayanga, kitamkosa Thomas Ulimwengu kutoka AFC Eskilstunaya Sweden.
Taarifa ambazo Mayanga amezipata
kutoka Sweden ni kwamba Ulimwengu kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa
madaktari wa timu hiyo ya AFC Eskilstuna. Hivyo sasa Mayanga atabaki na
washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ibrahim
Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu Shooting).
Mbali ya hao, nyota wengine
aliowataja Jumatatu iliyopita ni walinda milango, Aishi Manula (Azam
FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Walinzi wa pembeni upande wa kulia
aliwataja Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati
upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam
FC).
Mayanga aliwataja walinzi wa kati
Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba
SC) na Erasto Nyoni (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa
ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).
Kadhalika wako viungo wa
kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank
Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia
waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shiza Kichuya (Simba SC).
Viungo wa kushoto ni Farid Mussa
(Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati wasaidizi
wake ni Kocha Wa Makipa, Patrick Mwangata, Meneja wa timu, Danny Msangi,
Mtunza Vifaa Ally Ruvu wakati Daktari wa timu atakuwa Richard Yomba
huku Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza na
Botswana Machi 25, 2017 kabla ya kuivaa Burundi Machi 28, mwaka huu
katika michezo kirafiki wakati huu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa
la
Mpira wa Miguu (FIFA).
Mpira wa Miguu (FIFA).

0 Comments