Kesho ni siku ya Jumanne
Shirikisho la Mpira barani Afrika CAF linatarajia kutoa ratiba ya
kuwania kuingia hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho ambapo timu ya
Yanga inatajua inakutana na timu ipi hii ni baada ya kuondoshwa Ligi ya
Mabingwa
Droo hiyo itakayoanza kupangwa mchana katika mji wa Cairo nchini Misri na itahusisha timu zilizovuka hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho dhidi ya zilizotolewa kwenye hatua hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu zilizotolewa Ligi ya Mabingwa zitamenyana na zilizosonga mbele Kombe la Shirikisho katika mechi za nyumbani na ugenini kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani.

Mechi za kwanza zinatarajiwa
kucheza wikiendi ya Aprili 7 hadi 9 na marudiano yanatarajiwa kuwa
wikiendi ya Aprili 14 hadi 16, mwaka huu.
Timu zilizovuka hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho ni MC Alger, JS Kabylie za Algeria, Recreativo do Libolo ya Angola, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, El Masry, Smouha ya Misri, MAS Fes, Ittihad Tangier za Morocco, Rayon Sports ya Rwanda, Hilal El Obeid ya Sudan, Mbabane Swallows ya Swaziland, Platinum Stars, Supersport United za Afrika Kusini, Club Africain, CS Sfaxien za Tunisia na Zesco United ya Zambia.
Zilizotolewa Ligi ya Mabingwa ni RC Kadiogo ya Burkina Faso, AC Leopards ya Kongo, AS Tanda ya Ivory Coast, TP Mazembe ya DRC, Gambia Ports Authority ya Gambia, Horoya ya Guinea, CNaPS ya Madagascar, AS Port Louis ya Mauritius, FUS Rabat, Wydad Athletic Club ya Morocco, Ferroviario Beira ya Msumbiji, Rivers United, Rangers ya Nigeria, Bidvest ya Afrika Kusini, Yanga SC ya Tanzania ya KCCA ya Uganda.

Hivyo kuna wasiwasi kipindi hiki
Yanga watakutana na timu ya kiarabu ambazo zinaonekana ni nyingi ambazo
zimeingia hatua ya mtoano na ni jukumu la benchi la ufundi pamoja na
wachezaji kujua nini cha kufanya kwani mwaka jana walitolewa na Al-Ahly
na kuangukia kwenye hatua hiyo ambapo walifanikiwa kuingia hatua ya
makundi japo hawakufanya vizuri

0 Comments