Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Constantine Mushi akizungumza na
wahitimu kabla ya kufunga jana mafunzo hayo fani ya Utalii na Ukarimu
yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika
Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya wahitimu
74. Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki
(kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskaz Mwiru (kulia)
Mmoja wa Wahitimu wa mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji
huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na
Ukarimu, Lyimo Leb akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi kabla ya
mafunzo hayo kufungwa.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii,Jesca William
akiwaonesha baadhi ya video zinazotumika katika kutoa mafunzo ya
mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika
fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na
Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu.
Baadhi ya wahitimu waliohitimu jana mafunzo katika maeneo ya
mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika
fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na
Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na
kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74.
Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki
akizungumza na wahitimu waliohitimu jana mafunzo katika maeneo ya
mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika
fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na
Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na
kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74.
Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskaz Mwiru akizungumza
na wahitimu kabla ya kufungwa mafunzo hayo jana katika maeneo ya
mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika
fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na
Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na
kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74.
(Picha na Lusungu Helela- WMU)
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Constantine Mushi akikabidhi cheti
kwa Mwenyekiti wa wenye hoteli katika mkoa wa Mbeya, Jeremiah Mchange
cha ushiriki wa mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya
chakula na vinywaji pamoja na upishi
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi akiwa kwenye
picha ya pamoja mara baada ya kufunga mafunzo ya jumla ya wahitimu 74
waliopewa mafunzo ya siku tatu katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma
ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na
Ukarimu. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na
SPANEST Mkoani Mbeya, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa huduma
zinazotolewa katika sekta hiyo ili kukidhi mahitaji ya soko, pamoja na
kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya kiwango. Wengine ni
Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki (kushoto)
Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskas Mwiru (kulia)
.........................................
Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya
Utalii, Paskaz Mwiru akizungumza na wahitimu kabla ya kufungwa mafunzo
hayo jana katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na
vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu
yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika
Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki
74. (Picha na Lusungu Helela- WMU)
…………………..
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Constantine Mushi amewataka wamiliki wa hoteli kuajiri wafanyakazi wenye
ujuzi katika fani ya ukarimu na utalii baadala ya kuajiri ndugu zao
wasio na ujuzi wowote na kuwalipa ujira mdogo hali inayochangia
kuzorotesha huduma za utalii mkoani hapo.
Alisema wahudumu walio wengi
katika hoteli hizo wamekuwa kero katika utoaji wa huduma kwa watalii
pindi wanapotembelea kuja kuona vivutio vya utalii vilivyopo mkoani
hapo.
Ametoa raia hiyo jana wakati
akifunga mafunzo hayo kwa jumla ya wahitimu 74 yaliyoandaliwa na Wizara
ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST
unaotekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Amesema mafunzo hayo
yamefanyika kwa muda wa siku tatu kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma
zinazotolewa katika sekta ya ukarimu na utalii ili kukidhi mahitaji ya
soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya
kiwango kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini.
Amesema Wahitimu hao wamepewa
mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji
pamoja na upishi kwa ufadhili wa asilimia 75 uliofanywa kupitia mradi wa
SPANEST
Aidha, Mushi alisema kwa
kutambua umuhimu wa sekta ya utalii tayari umejipanga katika kuboresha
sekta ya utalii ambapo kwa mkoa wa Mbeya imeshaandaa Mpango Mkakati wa
kuendeleza utalii .
Kwa upande wa Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Utalii, Paskas Mwiru amesema mafunzo hayo yatakuwa
endelevu kwa wahudumu na pamoja na wamiliki wa hoteli ili waweze
kutambua umuhimu wa wafanyakazi wao.
Naye, Mratibu wa Mradi wa
SPANEST, Godwell Mengiaediek amewataka wahudumu wa hoteli waunde chama
chao ambacho kitawasaidia katika kupaza sauti zao.








0 Comments