Mifuko 50 ya saruji iliyochangiwa na mbunge wa jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete, na mifuko 50 aliyochangia diwani wa kata ya Vigwaza
Mohsin Bharwani kwa ajili ya ujenzi wa madarasa sita shule ya msingi
Vigwaza. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Katibu wa Mbunge Ridhiwani Kikwete, bw. Iddi Swala akizungumza na wakazi
wa kijiji cha Vigwaza kuhusu utekelezaji wa mfuko wa jimbo na Ridhiwani
alivyosaidia kijiji hicho na kata kijumla.
(picha na Mwamvua Mwinyi)
Diwani wa kata ya Vigwaza, Mohsin Bharwani ,akiteta jambo na mkazi wa
kata hiyo baada ya kuchangia mifuko ya saruji 50 kwa ajili ya ujenzi wa
vyumba sita katika shule ya msingi Vigwaza .
(picha na Mwamvua Mwinyi)
...................................
Na Mwamvua Mwinyi,Vigwaza
WAKAZI wa kijiji cha Vigwaza,Kata ya Vigwaza,jimbo la
Chalinze,wameanza kuchangia matofali matano kila mmoja na kujitolea
nguvu kazi ili kujenga vyumba vitano vya madarasa na chumba kimoja cha
chekechea katika shule ya msingi Vigwaza.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ramadhani Kirumbi, alisema
serikali ya kijiji imekubaliana na wananchi kuongeza majengo shuleni
hapo.
Kutokana na juhudi hizo, mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi
Evarist Ndikilo, alieleza anatambua jitihada za wananchi hivyo atawaunga
mkono kwa kuchangia sh. Mil mbili.
Mhandisi Ndikilo, alisema jamii ishirikiane na serikali kwa
kutatua changamoto za kijamii hasa elimu ili kuwajengea mazingira bora
wanafunzi.
"Tulijikita kwenye kuondoa matatizo ya uhaba wa madawati
lakini kwasasa haina budi tujiongeze kumaliza changamoto ya majengo na
madarasa "alibainisha .
Nae mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, alichangia mifuko ya saruji 50 na mabati 50 yenye thamani ya mil. 1.9 .
Katibu wa mbunge huyo Iddi Swala,alisema Ridhiwani
amechangia pia zahanati ya kijiji kipya cha Mnindi mifuko 50,ukarabati
nyumba ya mwalimu shule ya msingi Mnindi mifuko 30.
Hata hivyo, Ridhiwani alitoa mifuko mingine 30 kwa ajili ya kufanya ukarabati zahanati ya Kitonga.
Katibu Swala, alieleza kwamba, mh mbunge kapeleka mifuko ya
saruji mingine 50 katika shule ya msingi Milo na zahanati ya Buyuni
ametoa mifuko 30 ya saruji.
"Kati ya fedha za jimbo mil 48 kata ya Vigwaza imechangiwa mil. tano "alisema Swala kwa niaba ya Ridhiwani.
Diwani wa kata Vigwaza,Mohsin Bharwani, alitoa mifuko 50 ya
saruji na taasisi ya lions Dar es salaam -Panorama imesaidia mifuko ya
saruji 50.
Bharwani alisema kwasasa, katika sekta ya elimu wanajikita kumaliza tatizo la upungufu wa madarasa kwenye shule mbalimbali.
Bharwani alisema kwasasa, katika sekta ya elimu wanajikita kumaliza tatizo la upungufu wa madarasa kwenye shule mbalimbali.



0 Comments