Wanafunzi
wauguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright na SUZA wakiwa katika darasa la kufanyia
mazoezi ya vitendo wakielekezana namna ya kumuhudumia mgonjwa alielezwa wodini.
Kaimu Mkuu
wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)
Amina Abdulkadir akizungumza na wanafunzi wauguzi wa Chuo Kikuu cha Wright
Jimbo la Ohayo nchini Marekani walipotembelea Skuli hiyo Mbweni kubadilishana uzoefu.
Mwanafunzi
Muuguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright nchini Marekani Melissa Vanscoy akieleza
lengo la ziara yao hapa Zanzibar wakati
wanafunzi wa vyuo hivyo viwili walipokutana katika Skuli ya Afya na Sayansi za
Tiba ya SUZA Mbweni.
Wanafunzi
wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakibadilishana mawazo na wanafunzi wenzao wa
Chuo Kikuu cha Wright kutoka Jimbo la Uhayo Marekani walipowatembelea skulini
kwao Mbweni.
Picha ya
pamoja ya wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakiwa
na baadhi ya walimu na wenzao wa Chuo
Kikuu cha Wright, Jimbo la Uhayo nchini Marekani wakiwa katika kempasi ya
Mbweni.
Picha na
Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.





0 Comments