Random Posts

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA KUMWAKILISHA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN TAMASHA LA PASAKA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akitangaza mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 16 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Msama amemtaja Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba kuwa ndiye atakuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

Ameongeza kuwa maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na karibu mambo mengi yako tayari kwa ajili ya tamasha hilo litakalofanyika pia katika mikoa kadhaa, Ambayo ni Simiyu, Dodoma Iringa, Mwanza na Geita.

Post a Comment

0 Comments