Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa
mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za
kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana
na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. KushotoniMkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha.Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki yaWatu wa Zanzibar (PBZ) Said
Mohamed Said akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye
kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu kwa njia
ya simu zitakazotolewa na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki hiyoKisiwani
Pemba. (wa pili kulia) ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada Salum. Wa pili kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin
pamoja na Mkuu wa
Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha. Hafla hiyo ilifanyika
katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Mhe. Mohamed Ahmadaakizungumza wakati
wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki
zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya
Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. KatikatiniMkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin na kushoto
ni Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha.Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Mhe. Mohamed Ahmada (wa pili kushoto)na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said
Mohamed Said wakizindua huduma za mtandao wenye kasi zaidi wa 4G wa
Zantel na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa
njia ya simu na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na Benki hiyo kisiwani Pemba. Wanaoshughudia
niMkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin
(kushoto) na Mkuu wa
Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha.Hafla hiyo ilifanyika
katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (wa pili
kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said
Mohamed Said wakipongezana mara baada ya uzinduzi wa mtandao wenye
kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu
zitakazotolewa kwa njia ya simu na Zantel kwa kushirikiana na PBZ kwa wananchi
wa kisiwani Pemba. Wanaoshuhudia niNaibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada (katikati), Mkuuwa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha
(kushoto) na Meneja wa Benki ya Watu wa Zanzibar-Pemba, Mohamed Musa.Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Mhe. Mohamed Ahmada (wa tatu kushoto) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (wa pili kushoto),Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha(kushoto)
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata
misingi ya Kiislamu
wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said (wa pili kulia) na Meneja wa Benki
ya watu wa Zanzibar-Pemba,Mohamed Musa (kulia) mara baada ya kuzindua mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki
zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya
Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Hafla
hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Mkurugenzi
wa Mikakati na Utendaji wa biashara wa Kampuni ya Zantel, Shinuna
Kassimakifafanua jambo kwa vyombo vya habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa
mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za
kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana
na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa wananchi wa kisiwani Pemba. Pamoja nae
niMkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha.Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Wachekeshaji
kutoka kikundi cha Jufe-Pembawakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Rasilimali
watu wa Zantel-Zanzibar Bw. Omar H. Omar wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao
wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu
zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki
ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa wananchi wa kisiwani Pemba.Hafla hiyo ilifanyika
katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Pemba.
Kampuni ya mawasiliano ya ZANTEL imezindua mtandao wenye kasi zaidi wa 4G sambamba
na huduma za kibenki zinazozingatia kanuni za kiislamu kwa njia ya simu ikiwa
ni hatua ya kuboresha na kupanua huduma zake kwa wateja.
Katika hatua ya kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya simu,
Zantel imeshirikiana na BENKI ya watu wa Zanzibar (PBZ) katika kuhakikisha
wateja wake wanapata huduma zote za kibenki kama vile kuweka au kutoa fedha,
mikopo, kulipia ankara zao za huduma mbalimbali kama
vile maji, umeme au kununua vocha za simu n.k.
Akizindua huduma hizo kisiwani mwishoni mwa wiki kisiwani Pemba, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada alisema huduma hizo kutoka Zantel zimekuja
katika wakati muafaka kwa wananchi wa Pemba na kuongeza kuwa yeye na Wizara
yake wanaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na mitandao mingine ya simu katika kuhakikisha
huduma za simu zinaboreshwa zaidi visiwani humo.
“Uzinduzi wa huduma ya mtandao wenye kasi zaidi wa 4G
sambamba na huduma ya kibenki kwa njia ya simu ni vitu ambavyo wananchi wa
Pemba wamekua wakivisubiria kwa muda mrefu. Niipongeze Kampuni ya mawasiliano
ya Zantel kwa kulitambua jambo hili na kulifanyia kazi kwa haraka” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin
amesema uzinduzi wa huduma hizo mpya ni moja kati ya jitihada zinazofanywa na
kampuni yake katika kutoa huduma zenye ubora nchini ili kutimiza mahitaji mbalimbali
ya wateja wao.
Aliongeza kuwa huduma ya kibenki kwa njia ya simu za mkononi imewalenga
watu wote ila zaidi ikiwa ni jamii ya kiislamu kwani inazingatia kanuni na
misingi yote ya kiislamu wakati wa utoaji wa huduma.
“Pamoja na kurahishisha
huduma za kibenki huduma kwa njia ya simu, huduma hii pia itasaidia kuokoa
muda, ni huduma rafiki kwa kila mtu na yenye usalama mkubwa” alisema Benoit.
Kwa mujibu wa Taarifa za
Benki kuu ya Tanzania (BoT) ni kuwa watumiaji wa huduma za kifedha kupitia simu
za mikononi wamefanya miamala yenye thamani ya bilioni 988.9 katika kipindi cha
pili cha mwaka jana,huku mitandao ya simu ikigeuka kuwa njia muhimu katika
miamala ya malipo mbalimbali.
Janin aliendelea kuwahakikishia wateja wa Zantel kuwa kampuni
ya Zantel imekuwa katika ushindani kwa muda mrefu na kuwa bado wanaendelea
kuwekeza ili kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora zaidi kwa kiwango
kikubwa na teknolojia bora zaidi.
“Tutaendelea kufikisha huduma hizi kwenda sehemu mbalimbali
za hapa nchini, huu ni mwanzo tu kwa wateja wa Zantel ningependa wategemee
mambo mazuri zaidi”.
Kampuni ya Mawasiliano ya
simu ya Zantel, inaongoza kwa asilimia 80 kwenye soko la mitando ya simu kwa
Zanzibar na ndiyo kampuni ya kwanza kutambulisha huduma za kibenki kwa njia ya
simu hapa nchini.
Ni hivi karibuni tu ambapo, Zantel kwa kushirikiana
na Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) walizindua huduma mpya ya “Zantel
Madrasa” inayolenga kutoa mafundisho ya dini na kuwaunganisha wadau wa dini
hiyo kujifunza zaidi juu ya uislamu kwa kupitia simu zao za mikononi au
kujipatia jumbe mbalimbali na mawaidha ya kiislamu kwa kutuma ujumbe mfupi wa
maneno kwenda namba 15586.









0 Comments