Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye akikabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds
Media na Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa sakata hilo ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass leo Jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa tuhuma za
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia kituo cha Televisheni cha
Clouds Media ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan
Abbass (kushoto) akimwelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Moses Nnauye ushahidi wa CCTV uliombatanishwa katika CD aliyomkabidhi leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa
ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Hassan Abbass.
Katibu wa Kamati ya Kuchunguza Sakata la Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia ofisi za Kituo cha Televisheni cha Clouds Media,
Deodatus Balile akielezea yaliyomo katika ripoti yao kabla ya kumkabidhi Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nauye (kushoto) leo Jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Nape Moses Nnauye (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara
baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo
Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Dkt. Hassan Abbass na Katibu wa Kamati
hiyo Deodatus Balile.
Baadhi ya waandishi
wa habari wakifuatilia makabidhiano ya ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha
Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank
Shija – MAELEZO.






0 Comments