Faida ya Hifadhi endelevu ya Mazingira. Pichani
ni kibanda maalumu kwa ajili ufugaji wa vipepeo katika Kijiji cha Fanusi
Wilayani Muheza. Wananchi wa eneo hilo wamekua wakinufaika na uuzwaji wa
vipepeo hao nje ya chini na kuboresha hali zao za maisha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh. January Makamba akipanda mti aina ya 'Mnyasa' katika kuunga
mkono kampeni endelevu ya upandaji miti nchini, katika Msitu wa Amani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akimsikiliza Bw. Richard Kuyangana akiwasilisha maoni ya wananchi wa
Hale katika Mkutano wa Hadhara. Waziri Makamba amewataka wananchi hao kutii
sheria, kanuni na taratibu za hifadhi ya mazingira.
............................................
Ziara maalumu ya Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba kutembelea mikoa ya Kaskazini mwa
Tanzania yenye lengo la kung’amua changamoto za kimazingira, athari za
mabadiliko ya tabia nchi ili kuweka mikakati sahihi ya kukabiliana na
changamoto hizo, imeingi siku ya nne.
Hii leo Waziri Makamba
ametembelea Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, na kupokea taarifa ya hali ya
Mazingira Wilayani hapo taarifa iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi
MwanaAsha Tumbo.
Bi Tumbo ameainisha changamoto za
kimazingira katika Wilaya yake kuwa ni pamoja na kuwa ni pamoja na Uvuvi
haramu, Mabadiliko ya tabianchi ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na
shughuli za binadamu zisizozingatia uhifadhi endelevu ya mazingira ikiwa ni
pamoja na ukataji ovyo wa miti ya asili na misitu ya kupanda, kilimo cha
kuhamahama na uchimbaji wa madini katika kingo na pembezoni mwa vyanzo vya
maji.
Bi. Tumbo amesema kuwa hivi sasa
wilaya ya Muheza inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mvua kutoka misimu mitatu
kwa mwaka hadi kufikia msimu mmoja tu. "katika siku za hivi karibuni
kumekua na ongezeko kubwa la uchimbaji holela wa madini unaopelekea uharibifu
mkubwa wa mazingira". Ili kuimarisha doria kikamilifu wakazi wa Wilaya ya
Muheza wamewasilisha ombi maalumu la kujengewa nyumba za askari hii ni baada ya
kupata msaada kutoka United Nations
Development Programme ambao wamekubali kujenga kituo cha polisi.
Aidha, jitihada mbalimbali
zimechukuliwa na uongozi wa Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka zuio la
ukataji miti hovyo. Miti iliyopigwa marufuku ni pamoja na miti iliyooteshwa kwa
juhudi za watu binafsi na hata ile ya mashirika/taasisi. Kwa upande wake Waziri
Makamba ameupongeza uongozi wa wilaya hiyo
kwa juhudi za dhati za kuhifadhi mazingira, pia kuanzishwa kwa kampeni maalumu
ya kupanda miti. Jitihada nyingine ni pamoja na kufukia mashimo yote
yaliyochimbwa na wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu katika Kijiji cha Kihara,
katika msitu wa Amani.
Katika siku hii ya nne Waziri
Makamba alipata fursa ya kutembelea "Amani Nature Researve" ambapo
alishuhudia ni kwajinsi gani mazingira yamehifadhiwa na kuchangia kwa kiasi
kikubwa mradi wa kuzalisha vipepeo na kuuza nje ya nchi biashara ambayo imekua
ikiwasaidia wakazi wa kijiji hicho katika kusomesha watoto wao na kujenga
nyumba bora za kuishi.
Wakazi hao wa kijiji cha Kata ya
Fanusi walianisha changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa kuwa ni kukosa soko
la kuuza vipepeo hao baada ya kuzuiwa na Serikali. "Niwahikikishieni kuwa
suala hili tutalichukua na kulifikisha katika Wizara husika na naamini
litafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo" Makamba alisisitiza.
Nae Mhifadhi wa msitu wa Amani
Bi.Mwanaidi Kijazi ameainisha umuhimu huo
kuwa ni pamoja na hifadhi ya bionuai na mifumo ya ikojia, hifadhi ya
viumbe hai adimu duniani, maumbile ya asili maalumu kwa utunzaji wa vinasaba na
chanzo kikubwa cha vyanzo vya maji.
Ziara ya Waziri Makamba katika
mkoa wa Tanga hii leo imefanyika katika
Wilaya ya Muheza ambapo ameshiriki katika zoezi la kupanda miti, kutembelea
misitu wa Amani na kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kihara na
kuwasisitiza wakazi wa eneo hilo kutunza rasilimali zilizopo kwa manufaa ya
sasa na vizazi vijavyo.
Aidha, katika kuchangia shughuli za
maendeleo kijijini hapo Waziri Makamba ameahidi kununua miche ya miti 150,000
kwa ajili ya kuigawa maeno mbalimbali ya wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya
jitihada kwa wakazi hao kupanda miti kwa wingi kwa lengo la kulinda na kutunza
mazingira.



0 Comments