Mwenyekiti
wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna
wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (watatu kushoto), Katibu wa Bodi
hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi
wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani
(kushoto), wakati wajumbe wa Bodi hiyo walipotembelea nyumba za makazi za Makamishna
wa Uhamiaji, Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Bodi hiyo ilitoa wiki tano
kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo.
Katibu
wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mkurugenzi wa
Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya
Zabuni ya Wizara hiyo, wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua ujenzi
wa nyumba za makazi ya makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini
Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni
ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa
Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa
Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (kushoto) akiangalia kabati la nguo
katika moja ya chumba cha nyumba za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni
Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi hiyo walizikagua nyumba hizo na
kutoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi.
Mkuu
wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani akiwaonyesha Wajumbe
wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, nyumba za makazi za
makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wapili
kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala
wa Magereza, Gaston Sanga. Wapili kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi, watatu kulia ni Kamishna wa Fedha
na Utawala wa Uhamiaji, Peter Chogero, na kulia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Edwin Makene.
Mhandisi
wa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg ambayo inajenga nyumba za makazi za Makamishna
wa Idara ya Uhamiaji, Leonard Leonidace, akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi
ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, walipozitembelea nyumba hizo
wakikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo, hata hivyo Wajumbe wa Bodi
walitoa wiki kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Zabuni, Wizara hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza,
Gaston Sanga, na wanne kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa
Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (Katikati) na Katibu wa Bodi hiyo
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi (wanne
kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo, mara baada ya
wajumbe hao kumaliza ziara yao ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi za
Makamishna wa Idara ya Uhamiaji, zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata
hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni hiyo kukamilisha
ujenzi wa nyumba hizo.







0 Comments