Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini zaidi ya
milioni 65 kampuni tisa za simu nchini kwa kosa la kushindwa kukidhi
baadhi ya vigezo vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya kanuni ya
9,10 na 11 ya kanuni za ubora wa huduma za 2011
Akiongea jana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alizitaja kampuni hizo kuwa
Benson Informatics Limited Smart, Airtel Tanzania, Vodacom Tanzania,
Zanzibar Telecom Limited Zantel, Mic Tanzania Limited, Tigo, Viettel
Tanzania limited, Halotel, na Tanzania Telecommunications Company
Limited, TTCL huku akizitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatoa huduma
bora.
“TCRA inawakumbusha watoa huduma wote wa mawasiliano nchini
kuhakikisha mnatoa huduma zinazokidhi ubora wa sauti na upakuaji wa hali
ya juu (Kudownload) pamoja na kufuata sheria za huduma ya mawasiliano
ya mwaka 2011”. Alisema Kilaba
Aidha Mhandisi huyo alisema wataendelea kuwachukulia hatua wale
wote watakaoshindwa kukidhi vigezo vya ubora wa huduma kama ilivyo
agizwa.


0 Comments