Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) imefanikiwa
kuwasambaratisha Veterans wa Gymkana kwa ushindi wa mabao 3-1 katika
mchezo uliopigwa jana jini katika viwanja vya Gymkana, jijini Dar es
salaam.
Wakicheza kwa
kujiamini na uelewano mkubwa Maveterani kutoka Boko walionekana
kuutawala sana mchezo huo na kuwapa tabu wapinzani wao Gymkana
walioonekana kuicheza mechi hiyo kwa hofu.
Boko
waliianza karamu hiyo ya mabao mnamo Dakika Saba ya mchezo kufuatia
krosi maridadi toka kwa nyota wake machachari Malekano (messi wa Boko)
kutua kifuani kwa Charles Palapala na kuutupia nyavuni kwa ufundi
mkubwa, Goli hilo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Veterans wa Gymkhana waliokua wakiongozwa na
Nahodha Ally Mayai Tembele, Juma Pinto, Mohd Sebene na kiungo asiekabika
Makocha Tembele walilishambulia lango la Boko beach Veterans kama
nyuki na hatimae wakasawazisha kupitia kwa Mshambuliaji wao Mohd Sebene
baada ya beki wa boko Kitwana Mango kucheza rafu nje ya kumi na nane.
Baada
ya kusawazisha goli hilo, Timu ya Gymkana Veterans walionekana
kuridhika kimchezo na hivyo kuwapa nafasi Boko Beach kutawala kiungo
iliyokua ikiongozwa na Kudra Omary, Engenier Kamugisha, Elimboto Nkumbi
na Hebron Malakasuka na hatimae kuongeza magoli mawili ya haraka haraka
katika dakika ya 65 na 78 kwa magoli mazuri ya kiufundi yaliyowekwa
kimiani na Elimboto Nkumbi, huku goli la lingine likifungwa na beki
Mohamed Mwinchumu baada ya kazi nzuri iliyoanzishwa na kiungo Kudra
Omari.
Huo unakuwa ni
ushindi wa pili ndani ya siku saba baada ya mchezo wa kwanza kuirarua
Timu ngumu ya veteran ya AZAM magoli matatu kwa mawili.
BBV
watakua na kibarua kingine kigumu siku ya jumapili (Aprili 2) katika
uwanja wake wa nyumbani watakapo ikaribisha Timu nyingine ngumu ya Dar
City FC yenye nyota wa zamani kama George Masatu, Akida Makunda, Clement
Kahabuka, Ally Mpemba, Zubeir Zatwila, Salvatory Edwards na Kiungo
hatari Ernest Nyambo na Ally Kakima.


0 Comments