Chama cha soka duniani FIFA kimepanga kuwepo kwa michezo
sita ili zipatikane timu zitakazoingia katika fainali za kombe la dunia
mwaka 2020.
Rais wa shirikisho la
soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo
na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema.
FIFA
imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo
na ila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja
katika michuano ya mwaka 2026.
Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali.
Mapendekezo hayo yapo hivi
Afrika - 9 kutoka timu za awali 5
Asia - 8 kutoka timu 4 za awali
Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali
Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali
Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali
Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali
Hatua ya nyongeza ya timu hizo inatajwa kama sababu mojawapo ya kuonekana kwa nchi ambazo zilikuwa hazipati nafasi
Mwezi
januari chama hicho chenye mamlaka makubwa ya soka duniani, kilipanga
kuongeza timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia kutoka 32 mpaka
48 na hii itaanza mwaka 2026.

0 Comments