Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akiwasili
katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kwa ajili ya kula kiapo na kuanza majukumu
yake.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt
Jayaka Mrisho Kikwete akiwasili katika Viwanja vya Bunge kwa ajili ya
kushuhudia kiapo cha Mke wake Mama Salma Kiwete aliyeteuliwa hivi karibuni na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mbunge.
Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akisindikizwa
na wabunge wanawake kwenda kula kiapo cha kutumikia kazi yake leo Bungeni Mjini
Dodoma.
Mhe.
Salma Kikwete akila kiapo cha kuwa mbunge mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job
Ndugai leo bungeni Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala
Bora Mhe. Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha
kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao
cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani
akijibu hoja mbalimbaliz za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba
wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda
Mama Tunu Pinda akisalimia wabunge mara baada ya kutambulishwa kati ya wageni
wa Spika leo Bungeni Mjini Dodoma kushoto ni Mke wa Katibu Mkuu Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mama Devotha Gabriel.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera
Bunge Kazi Ajira na Watu wenye Ulemevu Mhe. Jenista Mhagama akitengua kifungu
cha Bunge kwa kuomba Bunge kuendesha shughuli zake siku ya Jumamosi na siku za
kazi kuendelea kwa awamu ya pili saa
kumi jioni badala ya saa kumi na moja jioni.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt
Jayaka Mrisho Kikwete akifuatilia shughuli za Bunge leo Mjini Dodoma.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.












0 Comments