Mkuu wa kitengo cha Kodi,
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi; Dennis Masami akitoa mada kuhusu Maana na Umuhimu wa ulipaji Kodi ya
pango la Ardhi kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Wizara hiyo.
.........
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imetoa tahadhari kwa wadaiwa wa kodi ya pango la Ardhi kwa
kutoa elimu ya kuhusu dhana ya Kodi hiyo.
Hivi karibuni Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa mafunzo mafupi kwa waandishi wa
habari kwa nia ya kuhamasisha ulipaji wa kodi ya pango la Ardhi na kubainisha
utofauti wake kati ya kodi hiyo na Kodi ya Majengo ambayo hukusanywa na Mamlaka
ya Mapato (TRA).
Akizungumza na waandishi wa
habari; Mkuu wa Kitengo cha Kodi; Dennis Masami alisema; Dhana ya ulipaji wa kodi ya pango la Ardhi inatokana
na Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999
katika fungu la 3 kifungu kidogo cha 1 (a) kinachosema: ‘Itambulike kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya
Umma iliyowekwa chini ya Mheshimiwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya wananchi’’
Aliendelea kusema kuwa; Mfumo huu wa umiliki wa ardhi
unatambulika kama lease hold na sio free hold,
ambapo aina hii ya umiliki ni upangaji katika ardhi, ambao mpangaji
anawajibika kufuata masharti ya upangishaji, mojawapo ya masharti hayo ni
kulipa pango la kipande cha ardhi. Ambayo Mmiliki ni Rais kwa niaba ya umma na
mpangaji ni Mwananchi.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi;
Mhe. William Lukuvi ametoa tahadhari kwa wasiolipa Kodi ya Pango la Ardhi akisema;
“Wale wote ambao hawajalipa Kodi ya Pango la Ardhi, wote wanao miliki viwanja na mashamba yaliyopimwa, wahusike
kulipa kabla ya mwisho wa mwezi wa sita (6). Ifikapo tarehe 30/06 hatua
zifuatazo zitachukuliwa dhidi yao; Watashitakiwa Mahakamani, Mali zao zikamatwe
na majengo yapigwe mnada kupitia madalali na Miliki zao zifutwe.
Alisema hatua hizo zote zitachukuliwa kwa mujibu wa
sheria, na kutoa tahadhari kuwa kila mmoja achukue hatua ya kulipa kwa hiari kwa
Maendeleo ya Taifa.
Na kitengo cha Mawasiliano
Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

0 Comments