Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi
Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na
mikakati waliochukua kukabiliana na kuondoa tatizo la maji machafu
yanayotoka jijini Tanga ili kuhakikisha maji yanarudi kwenye hali yake
ya kawaida lakini kulia ni Meneja wa Ufundi wa Mamlaka
hiyo,Farles Aram
Kushoto mwenye tisheti ya
njano ni Mwandishi wa Gazeti la Majira Mkoani Tanga,Mashaka Mhando
akiuliza swali katikati ni Joachim Kapembe kutoka Shirika la
Utangazaji la TBC na kulia ni Mwandishi wa ITV na Radio One Mkoani
Tanga,Wiliam Mngazija.
Mwandishi wa Habari wa
Gazeti la Citizeni Mkoani Tanga, George Sembony kulia akiuliza swali
kwenye mkutano huo kushoto ni Mwandishi Zawadi Kika wa Clous
TV
Afisa Uhusiano wa Mamlaka
ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo
kulia ni Mwandishi wa Gazeti la Citizeni George
Sembony
Mratibu wa shughuli za Mazingira
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga
Uwasa,Ramadhani Nyambukah akizungumza jambo kwenye mkutano
huo
Baadhi ya watumishi wa
mamlaka hiyo wakifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari
leo
Waandishi wa Habari Mkoani
Tanga wakichukua habari
Joachim Kapembe kutoka
Shirika la Utangazaji la TBCkushoto akiwa sambamba na mtumishi wa
mamlaka ya Maji Tanga Uwasa wakiingia kwenye kituo cha kusafishia Maji
cha Moye
Waandishi wa habari
wakitazama namna maji yaliyohifadhiwa kwenye kituo cha kusafishia maji
cha Mowe kabla ya kufika kwa walaji wa kwanza ni Sophia Wakati wa
Gazeti la Uhuru wa pili ni Mbaruku Yusuph wa gazeti la Tanzania Daima
Mwandishi wa Gazeti la
Mtanzania,Sussan Uhinga naye akiangalia namna maji yanavyosafishwa
kabla ya kuwafikia walaji
Waandishi wa Habari
wakiongozwa na Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania wakitembelea eneo la
kusafishia maji kabla ya kufika kwa watumiaji la
Eneo la Mowe ambalo maji
huchujwa kabla ya kuwafikia walaji
Mwandishi wa gazeti la
Mtanzania,Sussan Uhinga na Frank wa TK wakiwa kwenye eneo hilo
kujionea
Mratibu wa shughuli za
Mazingira wa Mamlaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah
akizungumza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu dawa ambazo
zinatumika kuwekwa kwenye maji
Mratibu wa shughuli za
Mazingira wa Mamlaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah
akiwaonyesha mitambo iliyopo kwenye kituo hicho wakati
walipoitembelea kujionea
Waandishi wakitoka kulia
ni Mashaka Mhando wa gazeti la Majira Mkoani Tanga kushoto ni William
Mngazija wa ITV na Radio One Mkoani Tanga
William Mngazija wa ITV na
Radio One Mkoani Tanga akiwa ongoza waandishi wengine kuingia kwenye
vyanzo vya maji kuona namna hali ilivyo
Mwandishi wa Habari wa
Gazeti la Citizeni Mkoani Tanga, George Sembony akiwa kwenye vyanzo
hivyo vya maji
Muonekano wa Maji kwenye
chanzo cha Maji cha Mto Zigi
MAMLAKA ya Maji na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa)inapoteza kiasi cha shilingi milioni 13 kila siku kutokana na kuongezeka kwa za shughuli za kibinaadamu zinazofanywa katika vyanzo vya maji vilivyopo katika Mto zigi na Muzii Wilayani Muheza.
Uwasa)inapoteza kiasi cha shilingi milioni 13 kila siku kutokana na kuongezeka kwa za shughuli za kibinaadamu zinazofanywa katika vyanzo vya maji vilivyopo katika Mto zigi na Muzii Wilayani Muheza.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kwenye
vyanzo vya maji,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira
Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alikiri kuwepo kwa
uharibifu mkubwa katika vyanzo hivyo unaosababishwa na wananchi katika
maeneo hayo.
Mhandisi Mgeyekwa alisema shughuli za uchimbaji wa dhahabu,kilimo na
maogesho ya mifugo katika vyanzo hivyo vimekuwa vikichangia kwa kiasi
kikubwa kuongeza matope kwenye bwawa la Mabayani linalosambaza maji
Mjini hasa kipindi hiki cha mvua za masika.
Aidha alisema kuwa awali mamalaka hiyo ilikuwa inazalisha maji kiwango
cha ujazo km 29,000 na kupungua hadi kufikia ujazo wa km 20,000 kwa
sasa jambo lililopelekea kuanza kutoa huduma hiyo kwa mgao ndani ya
Jiji la Tanga.
Alisema wao kama mamlaka baada ya kugundua kuwepo kwa tatizo hilo
walianza kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuvitembelea vyanzo vyote
vya maji ili kubaini uhalisi uliopo na namna ya kuanza kulishughulikia
jambo hilo kwa haraka zaidi ili lisiweze kuleta madhara kwa
wananchi.
“Ki ukweli tatizo hili la katizo la maji na maji kutoka machafu
haliwaathiri wananchi peke yake hata sisi kwenye maeneo yetu tunayokaa
limekuwa likijitokeza hivyo tunaangalia namna ya kupambana nalo usiku
na mchana kwa lengo la kutatua shida hiyo”Alisema.
Mkurugenzi huyo alisema tayari mamlaka hiyo imekwisha kuanza kuchukua
jitihada za haraka ikiwemo kutumia maji ya kisima cha mwakileo ambacho
kina uwezo wa kutoa maji kwa ujazo wa km 30,000 hadi 35,000 ambayo
yanaweza kukidhi mahitaji ya zaidi wananchi 47,000 kwa wakati mmoja
sambamba na kuzibua mabomba ambayo yamekuwa na tope iliyosababishwa na
mvua zinazoendelea sasa.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu
karibu na vyanzo vya maji kwani kufanya hivyo kunasababisha madhara
makubwa kwa watumiaji wake ikiwemo kupungua kina cha maji na maji
kutoka machafu jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
Akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari walio tembelea
vyanzo vya maji vya Mto Muzii,Zigi,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watumiaji
wa Maji Zigi Juu,Philipo Mdoe alisema hali ya uchafuzi wa maji na
kupungua kina kumechangiwa kwa asilimia kubwa na shughuli za
kibinadamu zinazofanywa karibu na vyanzo hivyo jambo ambalo jitihada
za haraka zisipochukuliwa kunaweza kukaleta athari zaidi kwa
wananchi.
“Tunaiomba mamlaka kwa kushirikiana na serikali kupitia vyombo
vya dola vifanye operesheni za kushtukiza mara kwa mara kwani hii
itasaidia kupunguza ama kuondokana na uchafuzi wa mazingira unaofanywa
na watu kwenye nyanzo hivyo “Alisema.
Awali akizungumza katika mkutano huo,Mratibu wa Mazingira Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Nyambuka
Ramadhani alisema suala la utunzaji wa vyanzo vya maji ni wajibu kwa
jamii kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri wa kuona namna ya kuvilinda
ili visiweza kuharibiwa.
“Lazima jamii itambua umuhimu wa kuvitunza na kuvilinda vyanzo vya
maji kwani bila hivyo wanaweza kukumbwa na athari za kukosekana kwa
maji au kupatikana kwa maji yasiyokuwa safi na salama hivyo
tushirikiana kupambana na waharibifu wa mazingira “Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
0 Comments