Dar es Salaam, Ijumaa Aprili 21, 2017;
Jumapili 23 April 2017 saa tano asubuhi, Macho na masikio ya watanzania
yataelekezwa jijini London, kumshuhudia mwanariadha wetu pekee
anayeshiriki mashindano ya London Marathon akifanya vitu vyake. Haya ni
moja ya mashindano maarufu zaidi ya riadha ulimwenguni
na yanashirikisha wanariadha wa viwango vya kimataifa kutoka nchi
mbalimbali kikiwemo Kenya na Ethiopia ambazo zina sifa kubwa katika
ulingo wa riadha.
Mashindano hayo yataonekana Mubashara kupitia king’amuzi cha DStv katika chaneli namba 209 ya SuperSport
(SS9) kuanzia saa tano asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande amesema kuwa kupitia king’amuzi maarufu cha
DStv kitaonyesha mashindano hayo mubashara hivyo watanzania wataweza kushuhudia wenyewe na wala siyo kwa kuhadithiwa.
“Wakati
wote DStv imekuwa kinara katika kuwahakikishia watanzania wengi uhundo
wa aina yake hususan katika
ulingo wa michezo na burudani na kwa mara nyingine tena tunauwezesha
umma wa watanzania kushuhudia tukio hili muhimu ambapo balozi wetu
Alphonce Simbu anatuwakilisha katika mashindano makubwa ya riadha”
akisema Maharage.
Alphonce,
ambaye ni Balozi maalum wa DStv, ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali
ya dhahabu katika mashindano
maarufu ya Standard Chartered Mumbai Marathon na anatarajiwa kuwapa
wakati mgumu manguli wa riadha ulimwenguni wanaoshiriki mbio hizi za
London.
Multichoice
Tanzania inamdhamini Simbu kwa muda wa mwaka mzima kwa lengo la
kufanikisha maandalizi yake
ya kushiriki katika mashindano ya Dunia yatakyofanyika jijini London
mwezi wa nane mwaka huu. Udhamini huu ulianza tangu mwaka 2016 ambapo
Multichoice humpatia Alphonce posho ya kujikimu pamoja na kusaidia kambi
yake ya mazoezi

0 Comments