Mchezaji wa JKT Ruvu Hassan Dirunga akiwa chini ya ulinzi wa Wachezaji wa Kagera Sugar.
Hassani tena akiwapa shida wachezaji wa Kagera Sugar
Rashid
Mandawa mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar akijiandaa kuingia wakati wa
kipindi cha pili cha mchezo huo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Vodacom.
Mchezaji
chipukizi Mbaraka Yusuph (kushoto wa Kagera Sugar akiambaa na mpira
huku beki wa JKT Ruvu akimkimbiza) kipindi cha pili.
Mbaraka Yusuph akilindwa na Wachezaji wa JKT Ruvu
Dakika 90 zilikamilika na Timu zote zilitoka bila kufungana, Kagera Sugar 0-0 JKT Ruvu.
Mchezaji hatari wa JKT Ruvu Hassan akiteta Jambo na Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime dakika 90 zilipokamilika.
Kocha
wa zamani wa Simba, Kagera Sugar/Ashanti United/ Abdallah King
Kibadeni(kushoto) akiteteta jambo na Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar
mtanange ulipomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kagera Sugar imetoka sare ya 0-0 na Timu ya JKT Ruvu.
Kikosi
cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya Timu ya JKT Ruvu leo
kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba na kutoshana nguvu kwa kutoka sare
ya 0-0.
| Kikosi cha Timu ya JKT Ruvu kilichoanza kupambana na Timu ya Kagera Sugar. |
Na Faustine Ruta, Bukoba
Ligi
Kuu Vodacom imeendelea tena Jumamosi na katika Uwanja wa Kaitaba
tukishuhudia Timu ya Kagera Sugar ikitoka sare tasa ya 0-0 dhidi ya Timu
ya JKT Ruvu inayoshikilia nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi kuu
Vodacom msimu huu.
Kikosi
cha Timu ya JKT Ruvu kinachonolewa na Kocha wa zamani wa Simba, Kagera
Sugar, Ashanti United na sasa JKT Ruvu King Kibadeni' kilionekana kukosa
mbinu kuifunga Timu ya Kagera Sugar kipindi cha pili baada ya kuonekana
kuwa na nguvu kwa kuingiza wachezaji waliokuwa na kasi kubwa.
Kagera
Sugar nao walikuwa wakifanya mashambulizi ya kila mara lakini
hawakuweza kupata bao lolote kwenye jitihada zao zote hizo za kipindi
cha kwanza na cha pili. Hadi kipindi cha pili kinalizika dakika 90
hakuna timu iliyoweza kumfunga mwenzake.

0 Comments