| Mkazi
wa Omukigusha akisaidiwa kuvutwa juu baada ya kuanguka shimoni asubuhi
leo kwenye mufda wa saa nne. Picha na habari na Faustine Ruta ......... |
Faustine Ruta, Bukoba
ZAIDI
ya watu 70 wameokolewa na Serikali baada ya kukumbwa na mafuliko
yaliyotokana na mvua iliyoanza kunyesha kuanzia saa 9 usiku.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo
wakati alipo hojiwa na waandishi wa habari katika Kata ya Bakoba mtaa wa
nyakanyasi.
Kinawilo alisema kuwa nyumba zote zilizoko kandokando ya mto kanoni zote
zimeathiliwa na maji kiasi kwamba tumetumia mitumbwi ya uvuvi kuvusha
watu.
“Niseme tu mpaka sasa hakuna kifo chochote kile Zaidi ya vitu kuhalibika kwa kulowa maji”alisema kinawilo
Aidha mkuu wawilaya alisema kuwa kuwa wananchi wachukue tahadhali pindi
mvua zinapo nyesha tu watoke nje ya nyumba kwa usalama Zaidi.
Naye Josefati Bonge mkazi wa Omukigusha alisema kuwa katika nyumba yake
hakuna kilichobakia kikiwa kizima kwani nimetoka mimi kama nilivyo na
ninamshukuru mungu familia yangu haikuwepo.
“Kiukweli kuna kila sababu ya kuhama maeneo kama haya maana nihatali kwa
binadamu mfano’ waliokuwa wamelala fofo wanahali gani hivyo kunatakiwa
kuchua hatua mapema ili kuhamia sehemu stahiki”alisema Bonge
Anitha Mziba mkazi wa Nyakanyasi alisema kuwa yeye katika familia yake
hakuna alie umia Zaidi ya vitu vyote vyandani hakuna kilichotoka.
“Yani
nimewabeba watoto wangu begani mmoja baada ya mwingine wakati huo mimi
maji yakiwa yamenifikia kwenye shingo kwakweli nihatali”alisema Mziba
Katikati ya Makazi ya watu Eneo la Nyakanyasi Mitumbwi imefanya kazi
Okoa okoa ikiendelea eneo la Nyakanyasi Mjini Bukoba leo hii
Wakaazi wa hapa Tangu usiku saa 9 waliondoka!
Eneo la Ziwa Victoria...Ufukweni
Prince Motel
Crane Lodge and Tours
Hii ni nyumba ya Wageni...lakini inasemekana Usiku hawakupata usingizi kabisa!
Patashika wakazi wakiokoa Nyasi kwa ajili ya Mifugo yao
Mkazi wa Nyakanyasi akivuka huku akiwa hana matumaini Aendako

0 Comments