Kaimu Kamishna Kitengo cha Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato hapa Nchini(TRA), Qamdiyay Akonaay (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo katika mkutano huo uliomalizika leo Aprili 27,2017.
Washriki wa mkutano huo wakiendelea kufuatilia
kilichokuwa kikiendelea.
Baadhi ya washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo
wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea.
Kamishna wa Forodha Nchini Uganda, Dickson c. (katikati) Kateshumbwa
akizungumza jambo katika mkutano huo.
Picha zote na Philemon Solomon
Picha zote na Philemon Solomon
Akisoma taarifa hiyo
mbele ya vyombo vya habari Kamishna wa Forodha Nchini Uganda, Dickson c.
Kateshumbwa amesema kuwa mkutano wa Umoja wa Forodha kwa nchi zilizo kwenye uanachama wa jumuiya ya
Afrika Mashariki hufanyika kwa zamu nchi
zote za uanachama. Ambapo kwa mwaka huu mkutano huo umefanyika hapa nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa kila mwaka mkutano huo hufanyika katika
ngazi tatu, ambazo ni ngazi zinayohusisha wataalamu wa masuala ya forodha ambao hutoka katika mamlaka za mapato za kila
nchi wanachama, na ngazi ya pili ni makamishna wote wa forodha walio katika
nchi wanachama huku ngazi ya tatu ni makamishana wote wakuu ambao jukumu lao
huwa ni katika kuidhinisha mipango na mikakati pamoja na kutoa maelekezo na
maagizo kwa ajili ya kuhakikisha mipango na mikakati inatekelezwa.
Alifafanua kuwa lengo la jumuiya ya
Afrika mashariki ni kuhakikisha
inatekeleza miradi mbali mbali ya forodha yenye lengo la kurahisisha na
kuhakikisha kuwa wafanyabiashara na wananchi wote wanapata faida kwa ujumla.
Naye Kaimu Kamishna Kitengo cha
Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato hapa Nchini(TRA), Qamdiyay Akonaay ametaja miradi iliyo katika mfumo huo wa
forodha kwamba ni pamoja na himaya moja ya forodha, muunganiko wa huduma za
kiforodha, kituo kimoja cha huduma Mpakani na wafanyabiashara wenye kuidhinishwa
huweza kupata huduma maalumu.
Mkutano huo ulianza Aprili 21 mwaka
huu na umemalizika leo Aprili 27 ambapo maazimio mbalimbali juu ya mkutano huo
yamejadiliwa na miongoni mwa hayo ni, mpango wa kuwa na himaya moja ya forodha,
muunganiko wa huduma za kiforodha na mapitio ya viwango vya ushuru na kanuni za
uasili wa bidhaa.





0 Comments