Random Posts

WAAJIRI TEKELEZENI SHERIA YA KAZI ILI KULINDA HAKI ZA WAFANYAKAZI-NAIBU WAZIRI MAVUNDE

 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson  akiongoza kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017.
 Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi na watu wenye Ulemavu  Mhe. Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017.
 Naibu Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Nyonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Rita Kabati akiuliza swali  katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Martha Umbula akiuliza swali  katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017.
 Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali (CHADEMA) akiuliza swali  katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017.
 Mbunge wa Kalenga (CCM) Mhe Mhe.Godfrey Mgimwa akiuliza swali  katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017.
 Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017.
 Mshindi wa Medali ya Dhahabu katika mbio za Mumbai za mwaka 2017 Bw.Alphonce Felix Simbu akiwaonyesha Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (hawapo pichani)  medali na Tuzo aliyoshinda katika mbio hizo leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe akipokea Tuzo kutoka kwa Mshindi wa Medali ya Dhahabu katika mbio za Mumbai za mwaka 2017 Bw. Alphonce Felix Simbu katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma.Wengine pichani ni Mkuu wa Utawala na Mafunzo JKT Col.K.J.Mziray,Luteni Col.J.P Meidini,Mkuu wa Kambi JKT Makuyuni Meja Mvula na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Multichoice Tanzania Bw.John Mshana.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akipokea Tuzo kutoka kwa Mshindi wa Medali ya Dhahabu katika mbio za Mumbai za mwaka 2017 Bw. Alphonce Felix Simbu katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma.Wengine pichani ni Mkuu wa Utawala na Mafunzo JKT Col.K.J.Mziray,Luteni Col.J.P Meidini,Mkuu wa Kambi JKT Makuyuni Meja Mvula na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Multichoice Tanzania Bw.John Mshana.


Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO,DODOMA
......
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Waajiri wote nchini yakiwemo makampuni ya Madini wametakiwa kutekeleza matakwa ya Sheria ya kazi kwa lengo la kulinda haki za wafanyakazi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi na watu wenye Ulemavu  Mhe. Anthony Mavunde wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Mjini Dodoma.

“Makampuni haya yana wajibu mkubwa wa kulinda haki za wafanyakazi,kupunguza migogoro isiyo ya lazima sehemu za kazi na kuongeza tija na uzalishaji mahala pa kazi.”Aliongeza Mhe.Mavunde.

Aidha amesema Ofisi yake imeendelea kutekeleza majukumu yake ya usimamizi wa Sheria kwa kufanya kaguzi sehemu za kazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa waajiri wanazingatia matakwa ya Sheria,elimu ya Sheria za kazi inatolewa kwa waajiri,wafanyakazi na vyama vyao ili kuongeza uelewa wao katika kutekeleza Sheria.

Kuhusu ukaguzi wa mikataba kwa kampuni zinazofanya kazi migodini amesema  Serikali iliunda kikosi ambacho kilishirikisha Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,NSSF,SSRA,OSHA ,Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wakala wa Ukaguzi wa Madini.

Amesema kikosi kazi hiki kilipewa jukumu la kufanya ukaguzi wa kina kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa na kaskazini kwa lengo la kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa Sheria za kazi,afya na usalama mahali pa kazi,masuala ya hifadhi ya jamii,fedha na kodi.

Pamoja na hayo amesema kuwa Serikali inatambua umhimu wa uwekezaji katika kukuza fursa za ajira kwa watanzania na kuchangia kukua uchumi kwa ujumla.

“Serikali itaendelea kusimamia sheria za kazi ili kuhakikisha kuwa waajiri wote nchini wanatimiza wajibu wao na wawekezaji wamepata nafasi ya kuwekeza na kuchangia kukua kwa uchumi wa nchi yetu kwa kufuata sheria zilizoko nchini”Alisisitiza Mhe.Mavunde.

Post a Comment

0 Comments