Wananchi wote mnatangaziwa kuwa kutakuwa na zoezi la kliniki
tembezi ya madaktari bingwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
kuanzia tarehe 3 April 2017 mpaka tarehe 7 April 2017. Madaktari bingwa
wa magonjwa ya akina mama, magonjwa ya macho, magonjwa ya ndani,
magonjwa ya meno, daktari bingwa wa upasuaji, magonjwa ya mifupa,
magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya masikio, pua na koo na magonjwa
ya watoto watakuwepo kuwahudumia kwa gharama nafuu sana. Wote
mnakaribishwa na atayeona tangazo hili tafadhali mjulishe na mwenzako.
Tangazo hili pia linapatikana katika tovuti rasmi ya mkoa wa Singida,
bonyeza www.singida.go.tz sehemu ya matangazo utaliona.

0 Comments