Kiungo wa Yanga,
Haruna Niyonzima, anaamini kabisa kama timu yake inataka kutetea ubingwa
wa Ligi Kuu Bara, ni lazima leo Jumamosi iifunge Azam FC kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga na Azam tangu
mwaka 2008, zimekutana mara 17 katika ligi kuu na zote zimeshinda mechi
tano kila moja na zimetoka sare mara saba. Yanga imefunga mabao 23 na
Azam imefunga mabao 22.
Katika msimamo wa
ligi kuu, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 53 nyuma ya Simba
iliyo kileleni na pointi 55, Azam ni ya tatu na pointi 44.
Niyonzima raia wa
Rwanda, amesema mchezo huo utakuwa mgumu kulingana na historia yao kila
wanapo-kutana lakini kwao ni muhimu kwani wakishinda watakuwa na mwanga
mzuri wa kutwaa ubingwa.
“Mechi yetu na Azam
ni mchezo mkubwa na utakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na kila
upande kuhitaji ushindi, lakini tumejipanga kushinda kwani ndiyo mechi
ambayo itatoa mwelekeo wa kutetea ubingwa wetu.
“Ni lazima tushinde
mechi hii ili tujiweke katika nafasi ya kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu
mfululizo, tuna majeruhi wengi lakini tutapambana ili tushinde,” alisema
Niyonzima.
SOURCE: CHAMPIONI

0 Comments