Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Chuo Kikuu
Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Lila Mandu akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) kuhusu Kongamano la Kimataifa la Jinsia na Usawa
Katika Jamii leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika
Aprili 27 mpaka 28 mwaka huu Chuoni hapo. Kutoka kulia kulia ni Mhadhri wa Chuo
Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Dorothea Fumpuni na Mratibu
Kitengo cha Jinsia DUCE Dkt, Fatma Hamad.
Mratibu Kitengo cha Jinsia DUCE Dkt, Fatma Hamad
akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Kongamano
la Kimataifa la Jinsia na Usawa Katika Jamii leo Jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Aprili 27 mpaka 28 mwaka huu Chuoni hapo
ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Samia Suluhu
Hassan. kulia ni Mhadhri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam
(DUCE), Dorothea Fumpuni.
Mhadhri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es
Salaam (DUCE), Dorothea Fumpuni akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari
(hawapo pichani) kuhusu Kongamano la Kimataifa la Jinsia na Usawa Katika Jamii
leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Aprili 27 mpaka
28 mwaka huu Chuoni hapo ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Kwanza
wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Kushoto ni Mratibu Kitengo cha Jinsia DUCE
Dkt, Fatma Hamad.
Baadhi ya waandishi
wa habari wakifuatiliaa mkutano baina ya wawakirishi kutoka DUCE kuhusu Kongamano
la Kimataifa la Jinsia na Usawa Katika Jamii leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano
hilo linatarajiwa kufanyika Aprili 27 mpaka 28 mwaka huu Chuoni hapo ambapo
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Picha na: Frank Shija
– MAELEZO
.....
Na
Husna Saidi-MAELEZO
Makamu wa Rais Mhe.
Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Kimataifa
la Jinsia na Usawa Katika Jamii
lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Aprili
27 mpaka 28 mwaka huu chuoni hapo.
Hayo yamesemwa leo
Jijini Dar es Salaam na Afisa Habari,
Elimu na Mawasiliano wa Chuo hicho Lila Mandu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu
lengo la kongamano hilo.
Mandu alisema lengo
kuu la kongamano hilo ni kuchunguza kwa kina masuala mbalimbali ya kijinsia pamoja
na kubaini mbinu bora za kuondoa ukosefu wa usawa wa jinsia katika muktadha wa
Taasisi za Elimu ya Juu.
“Tutatathmini sababu
na changamoto zinazosababisha ukosefu wa usawa wa kijinsia katika Taasisi za
Elimu ya Juu kwa kutumia mifano mizuri kutoka Taasisi zingine ambazo
zinajitahidi kuhamasisha usawa na haki za wanawake na wanaume pia,” alisema
Mandu.
Aliendelea kwa kusema
kuwa kongamano hilo litabainisha fursa za kimkakati katika kuwahusisha wadau wa
masuala ya jinsia katika kuhamasisha usawa na haki za watu wote ambapo litakuwa na washiriki 140.
Aliwataja washiriki
hao kuwa ni wasomi kutoka DUCE, Taasisi na vyuo mbalimbali ndani na nje ya
nchi, wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu katika masuala ya jinsia,
wawakilishi wa mashirika ya haki za binadamu, watunga sera pamoja na wasomi
wanaotambulika Kimataifa katika masuala ya jinsia.
Kwa upande wake,
Mratibu Kitengo cha Jinsia DUCE Fatma Hamad alisema licha ya maovu
wanayotendewa wanawake kuendelea kujitokeza hapa nchini, kongamano hilo
litasaidia kutoa elimu ya jinsia na usawa ili kusaidia Serikali na wananchi kwa
ujumla kuondokana na hadha hiyo.
Chuo cha DUCE pamoja
na waandaaji wa kongamano hilo wamealika wadau mbalimbali wa masuala ya jinsia,
wasomi, waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kushiriki katika kongamano
hilo.




0 Comments