Kamanda wa Usalama barabarani mkoani Pwani , Abdi Issango,akizungumza
na baadhi ya madereva wa magari wilayani Kibaha.
(Picha na Mwamvua
Mwinyi)
.............
Na
Mwamvua Mwinyi, Kibaha
KITENGO
cha usalama barabarani mkoani Pwani, kimeingiza sh.mil.867.810,kutokana na
makosa madogo 28,927,yaliyotozwa faini katika kipindi cha Jan-March 2017.
Fedha hiyo
imetokana na makosa hayo,ambayo yameongezeka , ukilinganisha na mwaka jana
kipindi kama hicho ambapo yalikuwa makosa 24,364.
Aidha
pikipiki zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali ni 4,226 ambapo zimesababisha
kukusanya sh.mil.126.780.
Kamanda
wa usalama barabarani mkoani Pwani, Abdi Issango aliyasema hayo,wakati akitoa
taarifa ya robo ya mwaka ya makosa ya usalama barabarani.
Alisema
Jan -march mwaka 2016 jumla ya makosa madogo 24,364 na mwaka huu yamefikia
makosa 28,927 ikiwa ni ongezeko la makosa 4,563.
Alieleza
kati ya pikipiki zilizokamatwa fedha hizo ni ongezeko la sh.mil. 146,610 ukilinganisha na fedha
iliyokusanywa Jan -march mwaka jana.
Hata
hivyo Issango,alisema kwa kipindi cha miezi mitatu sasa ,idadi ya ajali
zote,ajali za vifo na idadi ya watu waliokufa imepungua ukilinganisha na
matukio ya ajali za mwaka jana kipindi kama hicho.
Alifafanua,idadi
ya watu wanaokufa kwa ajali imepungua kutoka watu 80 katika kipindi cha
kuanzia januari hadi machi mwaka jana na kufikia watu 22 katika kipindi kama
hicho mwaka huu.
Alisema katika kipindi hicho idadi ya watu waliojeruhiwa katika ajali hizo ilipungua kutoka 181 hadi kufikia watu 32 .
“Pia kwa
kipindi hicho jumla ya ajali zote ilikuwa 162 na kwa mwaka huu wamefanikiwa
kupunguza hadi kufikia ajali 25 sawa na asilimia 84.56”alisema Issango.
Issango
alibainisha kwamba idadi ya ajali za vifo jan hadi march mwaka 2016
zilikuwa 70 kwasasa ni 20 pungufu ni 50 sawa na asilimia 71.42.
Awali
,mlezi wa kamati ya usalama barabarani mkoani humo ,ambae pia ni kamanda wa
polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga alisema pamoja na kupungua kwa ajali bado
kamati ya usalama barabarani ina kazi yakuendelea kutoa elimu.
"Kamati
hii kwa kushirikiana na kikosi cha usalama barabarani ina kazi kubwa ya
kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara wakiwemo
wanafunzi "
Kamanda
Lyanga alisema endapo watajenga umoja itasaidia kutokomeza suala zima la ajali
katika mkoa huo.
“Kila
mmoja asimame katika nafasi yake ,kila mtu achukie ajali,toeni elimu kwa
wananchi hasa kwa waendesha boda boda,wanafunzi ambao wamekuwa wakipoteza
maisha kwa ajali hizo”, alisema kamanda Lyanga.
Wakati
huo huo jeshi la polisi mkoani humo linamshikilia Paul Teremka(24),na Paul
Deogratius (22)walinzi wa Tiblus Michael (40)mkazi wa Mwenge,ili kusaidia
uchunguzi dhidi ya tukio la wizi wa ng 'ombe 40 waliokuwa kwenye zizi huko
Kerege kwa Kiwete Bagamoyo.
Kamanda
Lyanga, alibainisha katika tukio hilo watu wasiojulikana walivunja zizi na
kuiba ng 'ombe hao wenye thamani ya mil. 40.


0 Comments