Random Posts

MASHINDANO YA PIKIPIKI MAARUFU KAMA BODABODA KUFANYIKA MEI 13 MWAKA HUU JIJI DAR ES SALAAM.

Waandaji wa tamasha la bodaboda pichani kushoto ni  Meneja wa Kampuni ya  DP DECAUX Tanzania Ltd Shabani Makunga kutoka kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Elia Richard wakizungumza nawaandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo juu ya mandalizi ya shindano la "Dar es Salaam Bodaboda Super  Star".

PICHA NA PHILEMON SOLOMON

+255 656 525 666 / 0684 07 4444
.......
MASHINDANO ya Pikipiki maarufu kama bodaboda kufanyika Mei 13 Mwaka huu katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo kawe jijini Dar es salaam ambapo washiriki watatarajiwa kukimbia milimita 200 na jumla ya zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi ikiwemo Tv na Recorder.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo Mkurugenzi wa JP DECAUX Elia Rechard amesema fomu zaushirikizimesha anza kupatikana katika baadhi ya maeneo mbalimbali katika viuo vya boda boda ambapo ilikushiriki washiriki wote watatathiminiwa sifa zao ilikuweza kushiriki .

Amesema kuwa katika siku hiyo kutakuwa na wasaa baadhi ya washirirki watapatiwa mafunzo maalum ili kukuza uelewa washeria za barabarani itakayowezesha kupunguza ajali za marakwa mara katika maeneo mbalimbali nchini .

"Ilimshiriki aweze kushiriki mashindano hayo anatakiwa kuwa na leseni kama kigezo chakwanza chakushiriki mashindano hayo,kwani usafiri wabodaboda umekuwa njia rahisi za kumuwezesha msafiri kufika haraka hasa inapotokea dharur,"alisema Elia.


Amesema kutokana naumuhimu wahayo yote JP DECALUX kwakushirikiana na shirika la IRI (International Republican Instute) ambalo lisilo la kiserikali linalojiusisha na masuala ya maendeleo wameandaa tamasha hilo kama Dar Boda Boda Super Star Unity Festival .

Sambamba na hayo wadhamini wa tamasha hilo wametajwa kuwa ni Serengeti Brewries , SBC Tanzania Ltd kupitia kinywaji chake cha Pepsi ambapo pia kutakuwa na burudani kadha wa kadha burudani kutoka wasaanii wa kizazi kipya kutoka muziki wa Singeli ambapo mmoja wa wanaotarajiwa ametajwa kuwepo msanii Sharomwamba.

Post a Comment

0 Comments