Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni
(KUB), Mhe. Freeman Mbowe akihojiwa mbele ya ya kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge kufuatia amri ya Mhe. Spika wa Bunge ya kumtaka afike mbele
ya kamati hiyo kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka
ya Bunge kutokana na matashi yasiyo na staha aliyoyatoa mapema mwezi Machi 2017
Bungeni Mjini Dodoma yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mhe. Halima
Mdee (kushuto) akihojiwa mbele ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge
kufuatia amri ya Mhe. Spika wa Bunge ya kumtaka afike mbele ya kamati hiyo kujibu
tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na kutoa
matusi Bungeni na kumtukana Spika, matamshi aliyoyatoa mapema mwezi Machi 2017 Bungeni
Mjini Dodoma yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.
(PICHA
NA OFISI YA BUNGE)
0 Comments