Mjumbe
wa Kamati Kuu CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wajumbe wa kamati za Siasa
Tawi , wilaya na mkoa kwenye ukumbi wa TC Dunga, wilaya ya Kati
mkoa wa Kusini Unguja.
Kwenye
mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe 590 uliofanyika kwenye ukumbi wa
TC Dunga , Mhe. Samia aliwataka wana CCM kukiimarisha chama katika mkoa
wa Kusini Unguja , aliwaambia wajumbe hao kuwa CCMsi kadi CCM ni
Itikadi, ambapo aliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha
mafunzo ya itikadi mara baada ya chaguzi ndani ya chama kukamilika.
Alihimiza
Vijana waambiwe mambo mazuri ya CCM alisema "CCM peke yake, ndio
penye misingi,penye historia, na penye Malengo" na kutaka wananchi hao
kuunga mkono juhudi na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika kuleta maendeleo
nchini.
Mhe.
Samia pia alihimiza Makatibu kufanya kazi zao hasa katika kutoa taarifa
sahihi za masuala ya uchaguzi badala ya kubeba watu na alizitaka
Jumuiya kufanya kazi zake kwa mujibu wa kanuni na utaratibu.
Aidha
wakati wa kumkaribisha Mhe. Samia , Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Dkt. Abdalla Juma Mabodi alisema Wazanzibar wapuuze porojo za wanasiasa
waliopoteza muelekea kwani hata Jumuiya za Kimataifa zinaelewa CCM ndio
inayotawala kwa mujibu wa Sheria na Katiba na aliahidi kufanya kazi
zaidi na mashina.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdalla Juma Mabodi akihutubia kabla ya
kumkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa , Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa TC Dunga wilaya
ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.
Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa CCM Wilaya ya
Kati na wa Mkoa wa Kusini Unguja
alipowasili kwenye ofisi za CCM za
Wilaya ya Kati.






0 Comments