Wito
umetolewa kwa jamii ya watanzania kuacha mila potofu inayopelekea tabia
ya baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wenye matatizo mbalimbali hasa
tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi bali wawapeleke hospitali mapema
ili wapate matibabu kwani wanaweza kupona endapo wakiwahishwa
hospitali.
Wito huo umetolewa na Afisa Mawasiliano mwandamizi wa Hospitali ya Mifupa (MOI) Bi. Mary Ochieng, wakati akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Halotel walipotembelea wodi za watoto hao pamoja na kutoa misaada ya kijamii, akizungumza na wafanyakazi hao Ochieng, amesema kuwa licha ya Taasisi hiyo kufanya jitihada kubwa za kutoa elimu na kufanya upasuaji kwa watoto hao bure bado kuna baadhi ya wazazi wameendelea na tabia ya kuwaficha watoto wao.
“Tangu Taasisi yetu ichukue jukumu hili imefanya kazi kubwa sana, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumeweza kutoa matibabu kwa watoto wengi, ila changamoto kubwa bado inabaki kwa baadhi ya wazazi ambao wanawaficha watoto wao pale inapotokea wakagundua watoto wao wana matatizo ya vichwa vikubwa au mgongo wazi” Alisema nakuongeza.
Meneja
Mawasiliano wa kampuni ya simu ya Halotel, Stella Pius (kulia) na
wafanyakazi wenzake wakitoa zawadi kwa mmoja wa mama wa watoto wenye
matatizo ya vichwa vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa Taasisi ya
Mifupa Muhimbili (MOI)
“Bado
changamoto ziko nyingi sana ndani ya jamii ya Watanzania, Kwanza
wanawaficha watoto hawa, lakini pia wanawake wanao jifungua watoto wenye
matatizo wakati mwingine wananyanyaswa na wanaume wao au hata ndugu
kutokana na mila potofu zilizo ndani ya jamii yetu, sio jambo jema, na
sio sahihi kabisa ni lazima watoto wote wapewe haki sawa ya kuhudumiwa
kwani tunayo mifano ya watoto wenye matatizo haya na wameweza kupata
matibabu na sasa wanaendelea na masomo yao kama watoto wengine na pia
wana ndoto kubwa” Alisema Ochieng
Aidha ofisa huyo aliiomba,
Kamnpuni hiyo kuangalia namna ambavyo wanaweza kushirikiana na taasisi
hiyo katika kutoa elimu na kusaidia kuchangia gharama za matibabu kwa
watoto na wazazi wenye matatizo hayo kwani wengine wanatoka nje ya mkoa
wa Dar es Salaam na inakuwa vigumu wao kumudu gharama za maisha
wanapokuwa wanapokea matibabu.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi
Nguyen Van Son, alieambatana na wafanyakazi wa kampuni hiyo amesema
licha ya wao kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika sikuu ya pasaka, kwa
Pamoja kampuni yake itakaa na wataalam wa taasisi hiyo ili kuangalia
namna gani wanaweza kuwasaidia wagonjwa hao ikiwa ni pamoja na kufanya
kampeni ya kitaifa kusaidia kukabiliana na tatizo hilo.
“Tumeguswa
na tatizo hili hatutaishia kutoa misaada hii midogo ya kijamii, na
kuishia hapo lazima tuangalie kwa upana namna ambavyo tunaweza kuisaidia
serikali na jamii ya Kitanzania kupambana na tatizo hili kadri
tutakavyo weza,” Alisema Son.
Makamu
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel Pham Dinh Quan
(kulia) akiwaongoza wafanyakazi wenzake kutoa zawadi kwa mmoja wa mama
wa watoto wenye vichwa vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa Taasisi
ya Mifupa Muhimbili (MOI)
Wafanyakazi
wa kampuni ya simu ya Halotel wakiwa katika picha ya pamoja nje ya wodi
ya watoto ya Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) kabla ya kutoa zawadi
ya Pasaka kwa watoto hao.





0 Comments