Na Daudi
Manongi-MAELEZO, DODOMA
Serikali
imesema kuwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 vifaranga 67500 vilivyoingizwa nchini
kinyume na sheria viliteketezwa.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri, Wizara
ya Kilimo,Mifugo na Uvivu Mhe.William Ole Nasha leo Bungeni Mjini Dodoma
wakati wa Maswali na Majibu.
“Wako
wawekezaji wachache ambao hupewa vibali
maalum vya kuingiza mayai au vifaranga
wa kuku wazazi (Parents Stock) tu,ukaguzi kwa ajili ya kudhibiti uingizaji
vifaranga na mayai unaendelea na hatua kali zinachukuliwa kwa yeyote
anayekamatwa kwa kukiuka utaratibu”,Alisisitiza Mhe.Ole Nasha.
Amesema
kuwa kuanzia mwaka 2006 serikali iliweka
katazo la kuingiza kuku na mazao yake nchini ili kudhibiti ugonjwa hatari wa
Mafua ya Ndege na hakuna mwekezaji yeyote aliyeruhusiwa kupewa kibali cha kuingiza
vifaranga au mayai nchini kwa ajiri ya biashara.
Aidha
amesisitiza kuwa Sheria ya Magonjwa ya Wanyama na .17 ya mwaka 2003 na kanuni
zake za mwaka 2007 na 2010 zinatumika kudhibiti na kukagua uingizaji katika
maeneo ya mpakani,bandarini na viwanja vya ndege.


0 Comments