Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano
na Mazingira) kwa kushirikiana na wadau iko katika hatua za mwisho kukamilisha
Mkakati wa Taifa wa miaka mitano wa kupanda na kutunza Miti nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira)Mhe.Luhaga Mpina wakati akijibu hoja mbalimbali za
wabunge leo Mjini Dodoma.
“Tunaitaji kiasi cha shilingi bilioni 105 ambapo
kila mwaka tutatenga bilioni 20 kutoka
vyanzo mbalimbali vya Serikali na wadau wa maendeleo kwa ajili ya utekelezaji
wa mkakati huu ambao unaelekeza kila mwananchi,Taasisi za Serikali,Taasisi za
madhehebu,Asasi zisizokuwa za Serikali,kambi za Majeshi,Magereza,Shule na
makampuni kupanda na kutunza miti katika maeneo yao”,Alisema Mhe.Mpina.
Aidha amesema kuwa mkakati huu ni tofauti na
mikakati mingine iliyopita kwani kwa kushirikiana na Halmashauri zote nchini
itahakikisha kwamba miti inayopandwa inatunzwa na kukua na kuhakikishia
visababishi vinavyochangia miti kutokuwa vimebainishwa na mikakati ya
kuvidhibiti imeandaliwa ikiwa ni pamoja na upandaji wa aina ya miti kulingana na maeneo na utunzanji wa
miti hiyo.
Hata hivyo Serikali imekuwa ikitekeleza zoezi la upandaji
miti kote nchini kupitia Ofisi hii ambapo kila halmshauri inatakiwa kupanda
miti 1,500,000 kila mwaka na kuhakikisha inatunzwa nna pale itakapoonekana
inafaa Halmshauri zihahakishe maeneo ya wazi yanahifadhiwa ili kuruhusu uoto wa
asili kurejea.


0 Comments