Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi
Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamis kigwangalla akijibu hoja mbalimbali za wabunge
katika kikao cha nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini
Dodoma.
Na
Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Halmashauri zilizo katika maeneo ya migodi imeanza kuweka mikakati ya
kudhibiti magonjwa ya Kifua kikuu na Silicosis
kwa kutoa Elimu kwa wachimbaji wa
madini ikiwemo kujikinga na vumbi na kutumia njia sahihi za uchimbaji.
Hayo
yamesemwa na Naibu Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kingwangalla leo Bungeni Mjini
Dodoma wakati wa Maswali na Majibu.
“Tanzania
inafahamu changamoto ya uwepo wa magonjwa
haya ya kifua kikuu na Silicosis katika maeneo ya wachimbaji, kwa upande
wa Kifua kikuu tatizo hili ni kubwa lakini kuwekuwepo na ripoti za wagonjwa
wachache wa Silicosis katika hospitali
za Serikali ikiwemo Kibong’oto”,Alibainisha Mhe.Kigwangalla.
Ameeleza
kuwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Magonjwa ya
UKIMWI,Kifua Kikuu, na Malaria wa Global Fund to Fight AIDS,Tuberculosis na
Malaria nchi kumi wananchama wa jumuiya ya SADC ikiwemo Tanzania ziko katika
utekelezaji wa mpango wa kudhibiti kifua kikuu na magonjwa ya mfumo wa hewa
yatokanayo na uchimbaji madini ikiwemo Silicosis.
Aidha
katika mpango huo kuna afua itakayo
shughulika na sera za udhibiti wa vumbi
katika maeneo ya wachimbaji ambayo itawabana wachimbaji kudhibiti vumbi wakati
wa shughuli za uchimbaji.
“Serikali
itaongeza wigo wa huduma katika vituo vya afya kwenye maeneo yaliyoathirika ikiwemo Mkoa wa Geita ili vituo viwe na uwezo
wa kuchunguza na kutibu magonjwa haya na kuwajengea uwezo wataalamu wa afya
katika kuhudumia wagonjwa katika maeneo ya migodi”Alisisitiza Mhe. Kingwangalla.


0 Comments