Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji
Mhe. Charles Mwijage akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano
cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Na
Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa Rasimu ya Muswada wa
Sheria itakayoweka bayana taratibu na mfumo wa usimamizi na udhibiti wa bishara
ya chuma chakavu katika hatua mbalimbali za uzalishaji, ukusanyaji, usambazaji,
uuzaji na uyeyushaji wake kwa kuzingatia uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa
manufaa ya Taifa.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati
akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Biashara
ya Chuma chakavu imeshamiri hapa nchini na duniani kwa ujumla,na hili
limetokana na mahitaji ya vyuma chakavu ambapo kumetumiwa na wahalifu kuaharibu
miundombinu iliyojengwa kwa vyuma kwa nia ya kupata chuma ili waiuze kama chuma
chakavu”Alisema Mwijage.
Amesema
ili kukabiliana na hujuma hizi Mamlaka husika zikiwemo TANESCO, TANROADS na RAHACO wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na
jeshi la Polisi ikiwemo kutumia walinzi wa Taasisi husika ili kulinda
rasilimali hizo.
Amesisitiza
kuwa Muswada huu umeweka wazi na bayana adhabu itakayotolewa kwa mtu
atakayebainika kuharibu miundombinu.
Aidha
Mhe.Mwijage ametoa wito kwa watanzania kutoa taarifa pindi waonapo mtu
anayehujumu miundombinu kwa namna yote
ile.
“Natoa
wito kwa wenye viwanda na wafanyabiashara wa vyuma chakavu jiepusheni na
ununuzi wa vyuma ambavyo asili yake ina
mashaka na tutaharakisha sheria hii ili
kutatua tatizo hili”Aliongeza Mwijage.


0 Comments