Naibu Waziri wa Kilimo Uvuvi na Ufugaji
Mhe. William Ole Nasha akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano
cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Na
Daudi Manongi-MAELEZO DODOMA.
Serikali
imesema kuwa inaandaa utaratibu wa kuunda Bodi mpya ya wakurugenzi ya Tumbaku kwa kuwa ina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa
Sekta ya Tumbaku nchini.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.William
Ole Nasha wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge mjini Dodoma.
“Serikali
ilivunja Bodi ya Tumbaku kwa lengo la kufanya maboresho katika utendaji kazi wa
Bodi,na hatua hii ya kuvunja Bodi ya wakurugenzi haihusu kusitisha shughuli
zinazotekelezwa katika sekta hii ya tumbaku kwani wapo wataalamu wanaoendeleza
utekelezaji wa mpango uliopo wa kuendeleza zao la tumbaku”. Aliongeza Mhe.Ole
Nasha.
Aidha
amesisitiza kuwa upatikanaji wa pembejeo za zao hilo zitapatikana kupitia vyama
vikuu vya ushirika kwa kila eneo kwa kupitia mchakato wa zabuni unaosimamiwa na
kuratibiwa na vyama vikuu vya ushirika.
Amezitaja
pembejeo za muhimu kwenye zao la tumbaku kuwa ni mbolea aina ya NPK, Mbolea aina
ya CAN, nyuzi za kufungia tumbaku wakati wa kuvuna na wakati wa masoko zote
zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika.
Ameeleza
kuwa kwa kuzingatia kuwa wakulima wanahitaji huduma muhimu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea masoko
ya tumbaku kwa msimu wa 2017/18, Serikali imeateua timu kwa ajili ya uratibu na
kusimamia masuala hayo.
“Tuna
timu tayari iko mkoani Tabora ambayo itasimamia na kuratibu masuala mbalimbali
ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuandaa upatikanaji wa pembejeo kwa msimu
ujao,hivyo pamoja na WETCU kuvunjwa kazi za chama hicho zinaendelea kama
kawaida”Alisema Mhe.Ole Nasha.


0 Comments