Na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA
Serikali
kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvivu imesema imeshughulikia malalamiko ya wakulima wa Korosho kwa kuondoa makato
yasiyokuwa muhimu katika zao hilo.
Hayo yamesemwa
na Naibu Waziri Wizara hiyo Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu hoja mbalimbali
za wabunge leo Mjini Dodoma.
“Serikali
imekwisha fanyia marekebisho maeneo ambayo wakulima walikuwa wanalalamikia kwa kuondoa
kabisa makato hayo katika zao hilo”, Aliongeza Mhe.Ole Nasha.
Amesema kuwa
Serikali imefuta ushuru wa shilingi 20 kwa kilo kwa ajili ya chama kikuu cha
Ushirika,Shilingi 50 za usafirishaji wa Korosho,Shilingi 10 kwa kilo ajili ya
mtunza ghala na pia shilingi 10 kwa kilo kwa ajili ya kikosi kazi cha Masoko.Aidha
Sekta ina utaratibu maalum wa kupanga bei dira kwa kutumia vigezo
vinavyokubaliwa kwa pamoja na wadau wote.
Kwa upande wa
manunuzi ya pembejeo za korosho amesema hufanywa kwa pamoja na vyombo rasmi
ndani ya Tasnia ambapo awali ilikuwa ikisimamiwa na mfuko wa Maendeleo ya
Korosho na sasa Bodi ya korosho Tanzania.
Aidha ameeleza
changamoto zinazojitokeza katika kufikisha pembejeo hizo kwa wakulima wa
korosho na hatua zimechukuliwa kwa kushirikisha vyama vya ushirika ili
kudhibiti mianya ya pembejeo kwenda kwa wasio lengwa.
Pia Serikali
imeweka mfumo wa usambazaji wa pembejeo wenye lengo la kuhakikisha kwamba
pembejeo hizo zinawafikia walengwa pekee.
“Utaratibu huu
unazingatia kutambua wakulima wenye uhitaji na pembejeo na hununuliwa kwa
kutumia utaratibu wa ununuzi wa pamoja n akusambazwa kwa wakulima kwa kutumia
wakala walioteuliwa na kudhibitishwa na
Halmashauri husika”,Alisisitiza Mhe.Ole Nasha.

0 Comments