Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia)akimkabidhi
kitabu chenye Sheria Mbali mbali za Bunge Mhe. Douglas Syakalima (wa pili
kushoto), ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu na Kiongozi wa Msafara wa
kutoka Bunge hilo, Wabunge hao wamekuja kubadilishana uzoefu na kamati ya
kudumu ya Bunge ya Miundombinu katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika
Mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kulia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigala King.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waheshimiwa
Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu
kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge
ya Miundombinu, katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu, Mhe. Prof. Norman Sigala King akizungumza na Waheshimiwa Wabunge
kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka
Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya
Miundombinu, katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kaunda suti
nyeusi katikati)akipiga picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la
Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo
waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu
wakiongozwa na Mhe. Douglas Syakalima, ambae ni Mwenyekiti wa Kamati na
Kiongozi wa Msafara/Ujumbe huo katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika
Mjini Dodoma.
(PICHA
NA OFISI YA BUNGE)



0 Comments