Kamanda wa TAKUKURU Pwani, Suzan Raymond, akizungumza katika mkutano wa kutoa taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha July 2016-March 2017.
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
KAMANDA wa taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa(TAKUKURU)mkoani Pwani,Suzan Raymond,ameeleza kuwa taasisi hiyo imeokoa
kiasi cha sh.mil 81.245,katika kipindi cha July 2016-March-2017.
Amesema fedha hiyo imetokana na watumishi hewa
waliobainika mkoani hapo,ambao walikuwa wakilipwa mishahara kinyume na
utaratibu.
Aidha kamanda Suzan amesema,idara ya serikali za mitaa
hasa katika mamlaka za watendaji wa vijiji/mitaa/kata na polisi bado
zinaendelea kutafunwa na malalamiko yanayohusiana na rushwa.
Akitoa taarifa ya utekeleza kwa kipindi cha miezi
Tisa,alisema kwa kuzingatia maagizo kutoka mamlaka za juu,watumishi hao
walitakiwa kulipa fedha zote walizokuwa wakilipwa wakati wa utumishi tata.
Hata hivyo,alisema mafaili mawili ya watumishi 16
yamepelekwa makao makuu ya TAKUKURU kisha wataomba kibali kwa DPP kwa ajili ya
kufungua kesi kwa wale watakaobainika kuhusika na ubadhilifu wa fedha .
Kwa mujibu wa Suzan,maafisa utumishi hawahusiki moja kwa moja kusababisha watumishi
hewa kutokana na kuingiliana kwa majukumu baina yao na wakuu wengine wa idara
ikiwemo walimu wakuuu.
Kamanda Suzan alibainisha,katika kipindi hicho,ofisi hiyo
ilipokea malalamiko 363 kati ya hayo malalamiko 252 yanahusiana na vitendo vya
rushwa na uchunguzi wake unaendelea.
Alisema malalamiko 98 hayahusiani na vitendo vya rushwa
,ambapo walalamikiaji walishauriwa na wengine walisaidiwa kwa kuwasiliana idara
husika kwa lengo la kutatuliwa kero zao.
“Idara inayoongoza kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa
ni serikali za mitaa kwa malalamiko 135 hasa mamlaka za watendaji wa
vijiji/mitaa na kata ikifuatiwa na polisi yenye malalamiko 44”
Kamanda Suzan alifafanua ,mahakama malalamiko 43,idara ya
afya 26,ardhi 24,elimu 17,sekta binafsi malalamiko 17,baraza la ardhi
05,ushirika 11,maliasili 02 na kilimo 02.
Alisema malalamiko kwenye idara ya misitu 11,habari
01,TASAF 01 ,fedha 01,viwanda 01,mgambo 01,ujenzi 05,maji 05,madini 03,serikali
kuu 02,uvuvi 02,TAMISEMI 01,TANAPA 01 na kilimo 01.
Kamanda huyo alisema taasisi hiyo,imeshafungua kesi mpya
tatu katika mahakama ya wilaya na mkoa pia mkoa una kesi nne zinazoendelea
kusikilizwa,na wanatarajia kufuangua kesi kumi.
Kamanda Suzan alisema ,wanaendelea na majukumu yake kwa
kuelimisha umma,kufanya uchunguzi wa tuhuma zinazohusiana na vitendo vya rushwa
na uendeshaji wa mashtaka pamoja na kufanya uchambuzi wa mifumo .
“Lengo ni kubaini mianya ya rushwa na kutoa ushauri wa
namna ya kuiziba katika taasisi na idara mbalimbali kimkoa. takiwa kuzirejesha
kwa utaratibu uliokuwepo”alisema.
Nae mkuu wa dawati la sheria na mashtaka TAKUKURU mkoani
Pwani,John Sang’wa ,alielezea kuwa,wanatarajia kufikisha mafaili ya uchunguzi
wa watumishi hewa ambao tayari wamerejesha walizolipwa kama mshahara ,kwa
mwendesha mashataka mkuu wa serikali( DPP).

0 Comments