Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akimuwakilisha Makamu wa Raisi
Bi Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Masuala ya Usawa
wakijinsia ulioandiliwa
na Chuo Cha Ualimu (DUCE) jijini Dar Es salaam.
Prof Rwekaza Mukandala Makamu
Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar Es Salaam akihutubia wadau na wanafunzi waliojitokeza katika mkutano wa kwanza wa
masuala ya Jinsia na Usawa yaliyofanyika katika chuo kikuu cha Uwalimu DUCE jijini
Dar Es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof. William Anangisye akihutubia
jopo la Wadau na wanafunzi katika mkutano wa masuala ya Usawa na huku
akisisitiza wazazi na walezi kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.
Wadau
wa Masuala ya Usawa wa kijinsia wakifuatilia kwa ukaribu ujumbe uliokuwa
ukitolewa na Mh.Ummy Mwalimu Waziri wa Waziri wa
Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto aliyekuwa akimuwakilisha
Makamu wa Raisi Bi Samia Suluhu Hassan katika viunga vya Chuo cha Uwalimu DUCE
jijini Dar Es Salaam.
Picha
ya pamoja ya wadau wa masuala ya Usawa wakijinsia katika mkutano wa kwanza wa
masuala ya Usawa wakijinsia uliowakutanisha kujadili na kuhamasisha juu ya kumlinda mtoto wa kike ili apate Elimu
sawa kama ile apatayo mtoto wakiume katika jamii yetu.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba
wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao ili kufikia malengo walioyanayo
nchini.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
kwanza wa maswala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE)
alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri8 ya Muungano waq Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan leo jijini Dar es salaam.
“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo
pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni
tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa
wakati waliotarajia”alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa anaunga mkono
uamuzi wa Rais wa Tanzania Dkt. Jonh
Pombe Magufuli kwa kutoa elimu bure nchini kwani kunaongeza
idadi ya watoto wa kike kuwepo mashuleni
tofauti na kipindi cha nyuma.
Mbali na hayo Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi
kuwahamasisha watoto wao wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kukuza
rasilimali watu katika kujenga uchumi unaotokana na viwanda nchini.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof. William
Anangisye amesema kuwa lengo la mkutano
huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.





0 Comments