Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze ,Said Zikatimu akizungumza katika baraza la madiwani.
Madiwani na watendaji wa halmashauri ya Chalinze wakisikiliza jambo wakati wa kikao cha baraza la madiwani lililofanyika Lugoba .
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
HALMASHAURI ya
Chalinze,Bagamoyo ,mkoani Pwani imeiomba serikali kupeleka watumishi katika
idara ya afya na elimu ,mara baada ya utaratibu wa uhakiki kukamilika ,ili
kuziba pengo la upungufu wa watumishi 42 waliokumbwa na adha ya vyeti feki
katika halmashauri hiyo.
Aidha halmashauri hiyo
,imefanikiwa kutimiza malengo yake sita ndani ya kipindi cha miezi Tisa
,ikiwemo kuinua mapato yake ya ndani.
Hayo yaliyasemwa na
mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze, Said Zikatimu , wakati akizungumza
katika kikao cha baraza la madiwani,huko Lugoba .
Alielezea kuwa
,wameinua mapato hayo kutoka kiasi cha sh .mil 130 hadi kufikia sh.mil 390 sawa na asilimia 120 na kuwa ya
kwanza kimkoa.
Zikatimu alisema
,wameimarisha usimamizi wa makusanyo yao mbalimbali .
Alibainisha kwamba
,mbali ya hilo ,katika kipindi hicho wameshakopesha sh .mil 180 kwa vikundi vya
wanawake na vijana 58 vilivyopo kwenye kata za halmashauri hiyo .
Hata hivyo Zikatimu
,alieleza wanalipa wenyeviti wa vijiji na vitongoji sh .30,000 kila mwezi
kutoka katika mapato hayo .
"Wenyeviti hawa
wanafanya kazi kubwa hivyo tukaona ni vyema kuwalipa japo kiasi hicho kidogo
cha fedha " alisema.
Mwenyekiti huyo
,alisema pia kwa sasa hakuna mwananchi anaetozwa fedha za mafuta ya magari ya
wagonjwa kwenye vituo vya afya baada ya halmashauri kuamua kutenga fungu la
fedha ya mafuta kwenye vituo vya afya .
Zikatimu alisema
,katika miradi ya maendeleo wametenga asilimia 60 ya mapato yao ambayo hufanyia
mambo mbalimbali kama kujenga nyumba za walimu ,vyoo ,kununua matrekta na
mengineyo .
Kwa mujibu wake
,wanatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,kwa vitendo na wameomba
wananchi washiriki kulipa kodi na ushuru pasipo kukwepa .
Akizungumzia ishu ya
vyeti feki ilivyowaathiri,Zikatimu ,,alisema watumishi 42 wamekubwa na adha
hiyo kati yao 26 ni walimu ,watatu ni watendaji wa vijiji na waliobakia ni
idara ya afya .
Alisema zoezi hilo
limeathiri na halmashauri hiyo kwani awali kulikuwa na mapungufu ya walimu na
watumishi wa afya sasa kwa ongezo lililotokea changamoto ya upungufu wa huo
imekuwa kubwa.
"Wodi za uzazi
akina mama wajawazito wanapata shida ,wagonjwa wa dharura wanapata kero ,na
wanafunzi wamekuwa wakikosa kusoma kama inavyotakiwa " alisema Zikatimu .
Zikatimu aliipongeza
serikali kwa kubaini watu waliokuwa wakila mshahara kinyume na taratibu ambapo
ameiomba ,ione mapungufu yaliyoongezeka ili kupunguza ama kuondoa upungufu
uliojitokeza .



0 Comments