Afisa Mfawidhi wa kituo cha kulea Wazee cha
Kibirizi Bw. Heradius Mushi (kulia) akifafanua mambo mbalimbali yahusuo kituo
hicho kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(katikati) wakati
Kamishna huyo alipotembelea kituo hapo mapema wiki hii Mkoani Kigoma.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira
Mushi(katikati) akitoa maelekezo kwa Afisa Mfawidhi wa kituo cha kulea Wazee
cha Kibirizi Bw. Heradius Mushi (kulia) wakati wa ziara yake kituo hapo mapema
wiki hii Mkoani Kigoma kushoto ni Mkurugenzi wa Manunuzi kutoka Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ( Idara ya Ustawi wa Jamii) Bibi
Martha Chuma.
Mkurugenzi wa Manunuzi kutoka Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ( Idara ya Ustawi wa Jamii) Bibi
Martha Chuma pamoja na Afisa Mwandamizi Ustawi wa Jamii Kigendi Maige wakimsikiliza Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw.
Rabikira Mushi (hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo mabalimbai kwa uongozi
wa kituo cha kulea wazee cha Kibirizi Mkoani Kigoma alipotembeleaa kituoni hapo
mapema wiki hii.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi
akitia saini katika kitabu cha wageni mara bada ya kuwasili katika kituo cha
kulea Wazee cha Kibirizi mkoani Kigoma .
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi
akikabidhi baadhi ya zawadi kwa uongozi wa wazee waishio katika kituo cha kulea
wazee ya Kibirizi Mkoani Kigoma alipotembelea
kituoni hapo mapema wiki hii , kulia ni Mwenyekiti Bw. Said Lekegwa na kushoto
ni Katibu Bibi. Veronika Ramadhani.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(
wa tatu kulia) akizungumza na uongozi wa Wazee waishio katika kituo cha kulea
wazee cha Kibirizi Mkoani Kigoma watendaji kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto na uongozi wa kituo hicho alipowatembelea mapema
wiki hii.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi
akisalimiana na Katibu wa Wazee waishio katika kituo cha Kibirizi Mkoani Kigoma
Bibi. Veronika Ramadhani alipotembelea kituoni hapo mapema wiki hii.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Kigoma







0 Comments