Katikati Ni Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Mabodi
pamoja na viongozi wengine wakipeleka
bati kwa mafundi wanaoezeka
msikiti wa ijitimahi.
![]() |
| Msafara uliofuatana na Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala “Mabodi” wakionyeshwa maeneo mbali mbali ya Ijitimai hiyo.
NA
IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala
“ Mabodi” amewasihi viongozi na waumini
wa dini ya kiislamu kutumia fursa ya Ijitimai kuliombea taifa
liendelee kudumu katika hali ya Amani na Utulivu.
Nasaha hizo amezitoa mara baada ya kushiriki katika
shughuli za ujenzi wa Msikiti wa Ijitimai ya Kimataifa huko katika
kijiji cha Kidoto Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema
mamia ya waumini wa dini ya kiislamu watakaoshiriki katika ijitimai hiyo
watakuwa ni sehemu muhimu ya kufanya dua mbali mbali za kuimbea nchini
inusurike na maafa ili wananchi waendelee na shughuli zao za kijamii.
Alieleza
kwamba CCM inaunga mkono juhudi zinazofanywa na taasisi za kidini
nchini katika kuhubiri amani na mshikamano kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla.
Alisema
licha ya Chama hicho kuwa ni taasisi ya kisiasa bado kina jukumu kubwa
la kushiriki kikamilifu katika shughuli za kidini zinazoendeshwa na
wananchi wa wa itikadi tofauti za
kisiasa.
Aidha
kwamba Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kitatoa msaada wa kupeleka nguzo za umeme
katika nyumba ya wageni pamoja na kununua vifaa vya samani za ofisi ya jumuiya inayosimamia Ijitimai
hiyo ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Akitoa
taarifa juu ya maendeleo ya Ijitimai hiyo, Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh
Mwalim Hafidh amesema bado wanaendelea kumalizia ujenzi wa msikiti utakaochukua waumini zaidi
ya 5100 kwa wakati mmoja.
Alisema
bado wanakabiliwa na changamoto za upungufu wa vifaa vya ujenzi wa mabanda
yatakayotumika wakati wa Ijitimai pamoja
na ujenzi wa shule , chuo cha madrasa, hospitali na maktaba pamoja na miundombinu mingine nyingine ya
kijamii.
Aidha
ameupongeza uongozi wa CCM kwa ziara hiyo na kueleza kuwa taasisi nyingi za
kisiasa zimekuwa hazishiriki ipasavyo katika masuala ya kidini hali
inayosababisha kutokuwepo na ushirikiano mzuri kwa taasisi hizo.
Naye Makamo Mwenyekiti wa Jukumiya Fiysabilillah Tabligh Markaz Zanzibar,
Sheikh Wakat Hassan Bakar Alisema lengo la
jumuiya hiyo ni kukifanya kijiji hicho kuwa chimbuko la uislamu na ibada.
Naibu
Katibu Mkuu huyo ameambatana na baadhi ya ujumbe kutoka Baraza la Wazee CCM Zanzibar, Uongozi wa CCM Mkoa wa
Kaskazini Unguja na Mkuu wa Mkoa huo, Vuai Mwinyi Mohamed.
Ijitimai
hiyo inatarajiwa kufanyika Mai 19, mwaka huu na kuudhuriwa na wageni kutoka
nchi za Kenya, Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda, Ethiopia na Jamhuri ya
kidemokrasia ya Kongo.
|


0 Comments