Katibu wa CCM wilaya ya Kibiti ,Zena Mgaya akizungumza jambo.
Habari
-Picha na Mwamvua Mwinyi, Kibiti
WAKATI
serikali ikijipanga kuanzisha Mkoa wa kipolisi katika wilaya ya Rufiji, Kibiti
,Mafia na Mkuranga ,katibu wa CCM kata ya Bungu ,wilaya ya Kibiti, Halife
Mtulia amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana.
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kibiti, Zena Mgaya, alisema marehemu
ameuawa majira ya saa 4 usiku may 13 .
Alisema
alipata taarifa la tukio kutoka kwa viongozi wa CCM kata.
Zena
alieleza Mtulia ameuawa akiwa anatoka uwani mwa nyumba yake kwenda kuoga akiwa
ameshika ndoo ya maji ndipo wauaji wawili walipojitokeza na kumuua kisha
kutokomea kusikojulikana.
"Wauaji
hao walitumia usafiri wa pikipiki kwa kuiacha mbali na eneo la tukio na baada
ya kutimiza adhma yao walitembea kuifuata walipoipaki kisha kuondoka
"alielezea Zena.
Alisema
Marehemu alikuwa Katibu wa CCM Kata ya Bungu, Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM
Taifa kutoka wilaya ya Kibiti na mjumbe wa Serikali ya kijiji Nyambunda na
ameacha mke na watoto.
Zena
alisema kufuatia matukio ya mauaji kijiji cha Nyambunda kata ya Bungu
kimeshapoteza Mwenyekiti wa kiiji, Mtendaji wa Kijiji, na wenyeviti watatu wa
vitongoji vilivyoko katika kijiji hicho .
Alipoulizwa
kuhusiana na uchaguzi wa ndani ya chama unavyoendelea ngazi ya shina na matawi
Zena alisema wanachama wanagomea kujitokeza.
"Uchaguzi
wa safari hii ni mgumu hakuna anaejitokeza kugombea kabisa, watu wanahofu
"alifafanua.
Nae
Asha Hemed na Ramadhani Swedy walisema hali bado ni mbaya kiusalama katika
wilaya hiyo na Rufiji.
Walisema
jeshi la polisi lisambaze askari wake na maeneo ya vijijini ambako wahalifu hao
ndio wamejikita huko.
Matukio
hayo ni pamoja na Jan 19,ambapo mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nyambunda
,Oswald Mrope, aliuawa kwa kupigwa risasi.
March 1,mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Said Mbwana
aliuawa.
Octoba 24,2016 afisa mtendaji wa kijiji cha Nyambunda
Ally Milandu alipigwa risasi na kufa na novemba 6,2016 .
Tukio jingine ni lile la mwenyekiti wa kitongoji cha
Nyang'unda kijiji cha Nyambunda Mohammed Thabiti alipigwa risasi akielekea
kwake.
Jeshi la polisi Pwani limethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kudai , linaendelea kupambana na kuwasaka wahalifu na kuimarisha
ulinzi.

0 Comments