Miss
Tanzania namba mbili 2006 na Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate
Mwegelo akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule
ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza mtihani wao.
Miss
Tanzania namba mbili 2006 na Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate
Mwegelo akikabidhi cheti kwa wanafunzi
wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza
mtihani wao.
Kaimu Mkuu wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa akizungumza katika mahafali hayo
Jokate Mwegelo akizungumza katika mahafali hayo
Dada Mkuu wa shule ya Jangwani akimrisha keki Jokate katika mahafali hayo.
Na Mwandishi
wetu
Mwanamitindo,
muigizaji na Miss Tanzania namba mbili
2006, Jokate Mwegelo ametoa wito kwa watu maarufu nchini kusaidia kuondoa
changamotokatika sekta mbalimbali ili kupunguza mzigo serikali.
Jokate
alisema hayo wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya
Sekondari ya Jangwani ambapo jumla ya wanafunzi 118 walimaliza shule.
Mrembo huyo
ambaye ni Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa
Umoja wa Vijana wa Chama cha
Mapinduzi (UVCCM) amesema kuwa Tanzania ina watu wengi maarufu na wenye uwezo,
lakini wachache tu ndiyo wamekuwa wakijitolea kusaidia sekta mbalimbali
husasani elimu na afya.
Alisema kuwa
kwa hali ilivyosasa,ni vigumu kwa serikali kutatua matatizo yote na kuwaomba wanamuziki, wasanii, wafanyabiashara na viongozi
mbalimbali wa vyama na serikali kujitolea kusaidia kutatua matatizo katika
jamii.
Alifafanua
kuwa shule ya wasichana ya Jangwani ni kongwe
kutokana na kuanzishwa Mei 28, 1928, lakini mpaka sasa inakabiliwa na
matatizo mbalimbali wakati kuna wahitimu wengi ambao kwa sasa wana nyandhifa na
wanashindwa kuchangia.
“Mimi
sijasoma Jangwani, lakini niliguswa na matatizo ya viwanja vya michezo na
kuamua kujenga uwanja wa mpira wa kikapu na mpira wa pete (netiboli), nashukuru
viwanja kwa sasa vinatumiwa na shule zinazozunguka maeneo haya,naomba wengine
wasaidie, kuondoa changamoto zilizopo,” alisema Jokate.
Mrembo huyo
pia amewaomba viongozi wa serikali na wafanyabiashara waliosoma katika shule ya Sekondari ya
wasichana ya Jangwani, kusaidia kuondoa changamoto za shule hiyo.
Awali,
Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Amos Mgongolwa alisema mbali ya uchakavu wa majengo,
shule yao haina madarasa na mabweni ya kutosha, haina ukumbi wa kufanyia shughuli mbalimbali kama
sherehe na kulazimika kufanyia eneo la wazi, shule haina hata gari moja kwa
ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na matibabu kwa wanafunzi wenye
mahitaji maalum.
Mgongolwa
amesema wanafunzi wenye mahitaji maalum, ulazimika kutumia baiskeli za miguu
mitatu ili kwenda kwenye shughuli
mbalimbali za kimamoso nje ya shule.





0 Comments