![]() |
Watumishi wa Kitengo cha Kodi wakiwa Mkoani Arusha
katika zoezi la kusambaza Hati za madai.
|
Wamiliki wa Viwanja na Mashamba wakiendelea kujitokeza
kufanya malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi katika kituo cha malipo cha Ardhi
Street – Kivukoni.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi; Dennis Masami akielimisha
Umma kuhusu Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kupitia Televisheni /Azam TV
katika kipindi cha Morning Trumpet.
Mkuu
wa Kitengo cha Kodi; Dennis Masami akielimisha Umma kuhusu Ulipaji wa Kodi ya
Pango la Ardhi kupitia Radio/Radio Times FM katika kipindi cha Dira Yetu.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
imeendelea na zoezi la uhamasishaji wa Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi
nchini.
Wamiliki wa Ardhi wameendelea kujitokeza katika
kufanya malipo yao nchini kote.
Hatahivyo, Wizara inaendelea kuwakumbusha wale wote wanao
miliki viwanja na mashamba yaliyopimwa,
ambao bado hawajalipa Kodi ya Pango la Ardhi, wahusike kufanya malipo hayo
kabla ya mwisho wa mwezi wa sita (6), kwani Ifikapo tarehe 30/06 hatua
zifuatazo zitachukuliwa dhidi yao; Watashitakiwa Mahakamani, Mali zao
zitakamatwa na majengo yao kupigwa mnada kwa kupitia madalali na Miliki zao
zitafutwa.
Aidha, hatua zote zitakazochukuliwa dhidi yao zitakuwa
kwa mujibu wa Sheria. (Sheria
ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999, katika vifungu Na. 49 – 50).
Mwananchi Lipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa Maendeleo ya
Taifa Letu.
Na kitengo cha Mawasiliano
Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi




0 Comments