Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini
Unguja – Zanzibar akitokea mkoani Dodoma ambapo hapo kesho anatarajiwa kuzindua
ya kampeni maalum inayojulikana kama Mimi na Wewe mjini Unguja.
Lengo la
kampeni hiyo ni kuhamasisha jamii kuchangia kwa hali na mali katika uboreshaji
wa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, afya, mazingira na kusaidia watu
wasiojiweza katika Mkoa wa Mjini Magharibu, Unguja.
Katika
uwanja wa ndege wa Zanzibar, Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa
Mjini Magharibi Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud pamoja na Viongozi Mbalimbali wa
Serikali na wa Vyama vya siasa.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Unguja- Zanzibar
20-May-2017

0 Comments