Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akishirikiana na Viongozi wengine kufungua Gereza la Wanawake wilayani
Mpwapwa lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa
kushirikiana na wafungwa.Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa,
mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa
lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na
wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo
umefanyika wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mheshimiwa George Lubeleje , akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa lililojengwa na
wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo
limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya
Mpwapwa,mkoani Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa,
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa
lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na
wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo
umefanyika wilaya ya Mpwapwa,Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(wa pili kulia), akiongozana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dk. Juma
Malewa (kulia) kuelekea katika eneo lilipo Gereza la Wanawake Mpwapwa,
lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na
wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo
umefanyika wilaya ya Mpwapwa,mkoani Dodoma.
Wananchi wa Mpwapwa
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani
Mpwapwa lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana
na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65
.Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa,mkoani Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, MOHA
Serikali kupitia
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Benki ya Exim inatarajia
kujenga nyumba 9500 za askari magereza ili kukabiliana na changamoto za makazi
ya askari wa jeshi hilo hapa nchini.
Akizungumzia
changamoto za Makazi ya askari wa Jeshi la Magereza Nchini, wakati wa
uzinduzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alisema Serikali inatambua
changamoto za makazi kwa askari magereza na tayari iko katika mazungumzo na
benki ya Exim ili iweze kujenga nyumba hizo.
“Nawaomba
askari wetu nchi nzima wawe na subira Serikali inatambua na
inashughulikia changamoto ya makazi ya askari na tayari tuko katika
mazungumzo na wadau ikiwemo benki ya Exim kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba
takribani 9500, lengo ni kukidhi kiu ya makazi ya askari na familia zao,”
alisema Masauni.
Awali akitoa
maelezo ya ujenzi wa Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
Nchini, Dk. Juma Malewa alisema ujenzi wa Gereza hilo umefanywa na wataalamu
ambao ni askari Magereza kwa kushirikiana na wafungwa kama sehemu ya
utekelezaji wa amri ya Mh. Rais Dk. John Magufuli ya kutaka wafungwa
watumike katika kazi za uzalishaji ikiwemo kilimo, ujenzi na ufundi mbalimbali.
Ujenzi wa Gereza
hilo umegharimu jumla ya shilingi milioni 65 na litasaidia pia kuhifadhi
wafungwa 148 na hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa katika Gereza la Kongwa
mkoani Dodoma pamoja na kuepuka usumbufu wa ndugu wa wafungwa kusafiri
mpaka wilayani Kongwa kwenda kuwaona ndugu zao.






0 Comments