Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii, Zahoro Kimwaga akizungumza na vyombo vya habari juu ya warsha ya siku
moja iliyowakutanisha Wadau wa Utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika
jana mkoani Iringa ya kukusanya maoni ya
kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999
Mgeni rasmi, Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Fikira Kisimba (katikati) akizungumza na wadau wa Utalii wa Nyanda za Juu Kusini wakati
alipokuwa akifungua warsha ya siku moja iliyofanyika mkoani Iringa, Wengine ni
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kulia) akiwa na Mtaalamu Mwelekezi wa zoezi la ukusanyaji maoni ya
kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii kutoka
Economic Social Research and
Foundation (ESRF) Prof. Raphael Mwalyosi (kushoto)
Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii, Zahoro Kimwaga akifafanua jambo
kwenye warsha ya kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii iliyofanyika jana mkoani
Iringa ambayo iliwakutanisha wadau wa Utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Mdau wa Utalii akichangia maoni ya kuboresha Sera ya Taifa
ya Utalii katika warsha ya siku iliyowakutanisha wadau wa Utalii wa Mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika jana mkoani Iringa
Mdau wa Utalii akichangia maoni ya kuboresha Sera ya Taifa
ya Utalii katika warsha ya siku iliyoowakutanisha wadau wa Utalii wa Mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika mkoani Iringa
Baadhi ya Wadau wa
Utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu wakifuatilia mjadala wa utoaji maoni ya
kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 katika warsha iliyofanyika jana
mkoani Iringa
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu wa Mkoa wa Iringa,
(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Utalii wa Nyanda za Juu
Kusini mara baada ya kufungua mkutano wa
kukusanya maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 kwenye warsha
iliyofanyika jana Mkoani
Iringa. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga
(kulia) akiwa na Mtaalamu Mwelekezi wa Economic Social Research and Foundation
(ESRF) Prof. Raphael Mwalyosi (kushoto) pamoja na Prof. Amosi Majule (Picha na Lusungu Helela-MNRT
.....
Wizara ya Maliasili na Utalii imewataka Wadau wa Sekta ya Utalii wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutoa maoni na michango yenye tija
itakayopelekea upatikanaji wa Sera Mpya ya Utalii.
Sera hiyo
inatarajiwa kutoa majibu ya
changamoto za utalii wa sasa kwa sababu itagusia utalii nje ya hifadhi.
Kauli hiyo imekuja baada ya Sera ya Taifa ya Utalii inayotumika hadi hivi
sasa kufanyiwa mapitio kwa mara ya mwisho mwaka 1999 ambapo ni takribani miaka
17 iliyopita.
Hayo yameibainika kwenye warsha ya siku moja
iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na kuwatanisha wadau wa sekta
hiyo wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ili kukusanya maoni ya upungufu na
utekelezaji wake.
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga
alisema Sera na miongozo inayoongoza Sekta ya utalii imepitwa na wakati kutoka
na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yaliyotokea mfano, Serikali kujiondoa
katika umiliki na uendeshaji wa huduma za kitalii na kuachia sekta binafsi.
’’Si hayo tu sera ya awali haikuainisha vivutio
vyote vya utalii zaidi ya hifadhi pekee ambapo kwa sasa tatizo la ujangili na
mabadiliko ya tabia nchi yameathiri kwa kiasi kikubwa’’ alisema
Aliongeza kuwa, Sera mpya itakayoundwa itaweza
kwenda sambamba na aina ya utalii wa sasa ambao kipindi cha nyuma haukuwepo,
akitolea mfano utalii mikutano pamoja na utalii wa kiutamaduni ambao umekuwa
ukikua kwa kasi hapa nchini
Aidha, alifafanua kuwa wanahitaji miongozo mipya
itakayosimamia sekta hiyo ili kuondoa migongano ya kiutendaji katika taasisi
zinazohusika ikiwemo ya wanyamapori, misitu na uwekezaji ili kuendeleza utalii
na sio kudidimiza.
Akifungua warsha hiyo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Fikira
Kisimba allisema wameamua kupitia sera
hiyo kutokana na kasi ndogo ya maendeleo yanayopatikana katika sekta hiyo licha
ya kujaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii.
Kwa upande wake, Afisa Utalii wa Mkoa wa Njombe,
Amiri Abdi, alisema sera itakayoundwa iangalie namna ya kuweza kutumia
teknolojia rafiki ya kuvitangaza vivutio
vya vya Utalii vya Nyanda za Juu Kusini kwa kutumia gharama nafuu.







0 Comments