Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Manyara, Mhandisi Munis Weransari akifungua
warsha ya matumizi sahihi ya vipimo kwenye mazao iliyoandaliwa na
Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) na kufanyika mjini
Babati
Katibu Tawala Msaidizi Mkoani Manyara, (Huduma za Uchumi na Uzalishaji)
Felix Mwasenga akifunga warsha ya matumizi sahihi ya vipimo kwenye mazao
iliyoandaliwa na
Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) na kufanyika mjini
Babati .
Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania
(Mviwata), umelalamikia tozo, ushuru wa masoko na tozo za kusafirisha kwa gunia
badala ya kutozwa kwa uzito, kwani hujenga mazingira shawishi kwa wanunuzi na madalali
kuzidisha uzito wa vifungashi zaidi ya kiwango stahiki.
Mratibu wa Mviwata mkoani Manyara, Martin Pius
alisema hayo mjini Babati kwenye warsha ya uboreshaji matumizi ya vipimo na kuzingatia vipimo
sahihi vya ujazo na matumizi ya mizani wakati wa kufanya biashara ya mazao ya
kilimo.
Pius alisema lengo lao ni kutafuta hatua za
pamoja kwenye kuboresha biashara ya mazao ya kilimo kwa kuzingatia vipimo
sahihi vya ujazo ili kuongeza tija kwa wakulima, wanunuzi na halmashauri kwa
ujumla.
Alisema inatakiwa kuandaa mpango wa pamoja
unaotekelezeka kwa ajili ya kuwezesha matumizi ya vipimo katika wilaya ya
Babati
na
kupashana habari ya maboresho katika sheria ya vipimo, kanuni zake na
marekebisho yaliyofanywa.
“Matumizi
sahihi ya vipimo ni muhimu sana katika kuhakikisha uwazi na uhakika wa vipimo
vinavyotumika, ili wazalishaji, wanunuzi na watumiaji walindwe na serikali ikusanye
mapato inayostahili na takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo zipatikane,”
alisema.
Alisema tafiti zinaonyesha ukosefu wa
uelewa kuhusu vipimo sahihi siyo kwa wakulima au wanunuzi tu bali hata kwa
watumishi wa umma ambao wana dhamana kubwa katika kusimamia utekelezaji wake.
Alisema mazoea ya
kufanya biashara ya mazao ya kilimo bila kutumia vipimo sahihi yapo kila mahali
na kimsingi, biashara ya mazao ya kilimo inayofanyika mashambani hufanywa bila
kuhusika kwa wakala wa vipimo.
Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo
Weransari Munisi alisema ni vyema kutambua pia kuwa sio uzito tu wenye shida
katika biashara hii, bali hata vipimo vinavyotumika vinatofautiana kutoka eneo
moja na eneo jingine.
Alisema warsha hiyo ni ya muhimu
kutokana na mkazo unaowekwa na serikali kuzingatia vipimo sahihi vya ujazo
ikiwa ni pamoja na matumizi ya mizani wakati wa kufanya biashara ya mazao ya
kilimo.
“Ni
matazamio yangu kuwa wakala wa vipimo watajenga uelewa wa kutosha kuhusu sheria
husika na vipimo stahili kwa mazao ya kilimo na utajenga mtandao wa washirika
kudhibiti matumizi ya vipimo visivyo sahihi,” alisema Munisi.
Alisema uuzaji wa mazao mabichi
shambani ni kosa na hasara kubwa kwa wakulima kwani huwa hakuna kipimo cha
kupima mazao yaliyo shambani, na kunmkosesha mkulima mapato makubwa
yatakayopatikana na uuzaji wa mazao hayo pindi atakapovuna na kuuza kwa kutumia
vipimo sahihi vya ujazo.


0 Comments