Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wa Nyimbo za Mataifa mawili (Tanzania & Afrika Kusini) zikipigwa katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipita kukagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo
na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wakiangalia vikundi vya
ngoma za asili vilivyokuwa vikitumbuiza ndani ya viwanja vya Ikulu kwa Heshima
ya ugeni huo wa Rais wa Afrika Kusini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob
Zuma kabla ya kuanza mazungumzo yao Rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo
na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wakielekea kwenye ukumbi
wa mkutano kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Kimaendeleo yahusuyo
mataifa hayo mawili ya Tanzania na Afrika Kusini.
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipunga mkono wakati akiwasili Ikulu akiwa pamoja
na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuanza kuzungumza na wanahabari Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisoma hotuba yake wakati akizungumza na
wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni
wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuzungumza na wanahabari
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipiga ngoma wakati alipowasili Ikulu jijini Dar
es Salaam.
![]() |
Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza jambo na Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli![]() |
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mama Sizakele Zuma
Mke wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kufika ofisini kwake
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mama Sizakele Zuma Mke
wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyeambatana na msaidizi wake Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Vikundi
vya Matarumbeta vikitoa burudani wakati Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU




















0 Comments