Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa
Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 amefanya mazungumzo na
Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za
Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la
Dar es salaam
Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za
Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la
Dar es salaam wakifatilia kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa
Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg john Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa
Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 wakati wa kika na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za
Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la
Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa
Paul C. Makonda akisisitiza jambo
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Imebainika kuwa zipo kauli zisizo rafiki zinazotolewa Na watumishi wa
Umma dhidi ya wananchi katika Jiji la Dar es salaam wanaozuru katika
Ofisi mbalimbali kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali kutokana Na
mambo yanayowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa
Paul C. Makonda amebainisha hayo Leo Mei 18, 2017 Wakati akizungumza Na
Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za
Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la
Dar es salaam ambapo pia ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia katika
utendaji wao.
Mhe Makonda amesema kuwa mtumishi wa serikali
ambaye atabainika kutumia lugha ambazo sio rafiki kwa wananchi
atachukuliwa hatua za kinidhamu Mara baada ya kubainika kwani kufanya
hivyo ni kufifisha uaminifu wa wananchi dhidi ya serikali.
Sambamba Na hayo pia RC Makonda amesema kuwa Kazi ya watendaji
serikalini ni kutatua kero za wananchi japo wapo watendaji ambao
wamegeuka Na kuanza kuongeza migogoro badala ya kutatua.
Alisema
kuwa baadhi ya watumishi wa Sekta ya ardhi wanamiliki kampuni
zinazojihusisha Na mambo ya Ardhi Jambo ambalo kwa kiasi kikubwa
limekuwa likipunguza ufanisi katika utendaji kwani wanatumia muda mwingi
kufikiri kuhusu kampuni zao kuliko kuwatumikia wananchi serikalini.
Ametoa wiki moja kwa watumishi wote wanaomiliki kampuni hizi kuamua
moja ama kubali wakifanya Kazi serikalini Na kuachana Na kampuni binafsi
ama kubakia katika kampuni zao Na kuacha kazi serikalini.
"Watumishi hawa hutumia vifaa vya serikali kwenye miradi yao Jambo
ambalo hupelekea uchakavu Na uharibifu wa haraka wa vifaa vya serikali
hivyo zuio langu hili linajikita kuwataka watumishi wa Umma katika Mkoa
wangu kujikita katika utendaji wa shughuli za serikali" Alisema Mhe
Makonda
Alisema Ardhi Na Ujenzi ni moja Kati ya Idara zenye
matatizo mengi katika Mkoa wa Dar es salaam hivyo ametoa msisitizo
vibali vya Ujenzi kutolewa haraka ndani ya mwaka mmoja kwani
kuchelewesha kunapelekea wananchi wengi kujenga bila utaratibu.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ametoa maelekezo 17 ya
kuzingatia kwa watendaji wa Sekta hiyo ya Ardhi Na Ujenzi ambayo ni
pamoja Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Kushughulikia migogoro
ya ardhi Na Ujenzi ili wananchi wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu,
Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi
ndani ya mwezi mmoja Na zoezi hilo lianze Mwezi wa sita mwaka huu 2017
huku Mwanzoni mwa mwezi wa Saba kukitarajiwa kuzinduliwa teknolojia
ambayo wananchi watapata taarifa zao za Ardhi kwenye mtandao Jambo
ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani mwa wananchi.
Wakuu
wa Idara katika Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha wanatoa taarifa
kuhusu Mipango ya Idara kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia maafisa
habari kwani tayari wana mahusiano Na waandishi mbalimbali katika vyombo
vyombo vya habari, kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi yaliyotolewa
Hati, Na kujitokeza haraka kwa wote waliotoa Hati za maeneo ya wazi kama
wapo, kusimamia haraka upimaji wa maeneo yote ya Umma kama vile Shule,
Hospitali, Na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba Na
kutoa Mikakati wa Upimaji.
Maelekezo mengine ni pamoja Na Wakuu
wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha ufanisi Na bidii ya utendaji
inaongezeka hususani mikakati ya kuhusisha wapimaji binafsi
wanaotambulika kwani Mji ukipimwa vyema Madiwani watafurahi lakini pia
itakuwa njia rahisi ya kuepuka migogoro ya Ardhi, Kushughulikia
changamoto za kisera unaofanya utaratibu wa Upimaji Na utoaji wa Hati
kuchelewa kukamilka Na Mabaraza ya Kata kuangaliwa upya kwa mujibu wa
Sheria ili kuwa Na utendaji imara unaoshabihiana Na Jambo la kisera.
Pia Kila Mtumishi kufanya Kazi yake kwa Uaminifu kwani dhamana
aliyopewa ni kubwa Na anapaswa kuitendea Haki, Watumishi wote kusimamia
Na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani chama hicho
ndicho kimeingia mkataba Na wananchi katika kipindi cha miaka mitano,
Kila Mkuu wa Idara kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka
2015-2020 ili kutambua maelekezo yaliyobainishwa katika Sekta yake
sambamba Na kuwaelekeza wasaidizi wao pia kuisoma Na kuielewa vyema
ilani hiyo.
Kufatilia Na kufahamu upandaji wa madaraja Na stahiki
zao kwani ni Haki zao za msingi kisheria ikiwa ni pamoja Na kwenda
likizo, Watumishi wote kuheshimu mamlaka walizonazo Na kutumia vikao
halali kutoa taarifa sahihi kwa watu husika, Kuwa Na ushirikiano wa
watumishi katika Idara zote ili kukuza ufanisi wa Kazi Na Kujitokeza
ndani ya wiki moja kwa watumishi wote wa Sekta ya Ardhi waliojihusisha
Na utoaji wa Hati za Ardhi kinyume Na sheria. Na endapo wasipojitokeza
Na wakabainika watachukuliwa hatua za kisheria.
RC Makonda pia
ameelekeza wakuu wa Idara Kufafanua baadhi ya mambo ili Madiwani waweze
kuelewa Sambamba Na kutoogopa maadhimio kama wanatenda Kazi kwa mujibu
wa Sheria pasipo kupendelea, Wakuu wa Idara kila.




0 Comments